Wakati Chama cha Wananchi (CUF), kikiwa kimetangaza rasmi kutoshiriki uchaguzi mkuu wa marudio visiwani hapa, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema suala la chama cha siasa kushiriki au kutoshiriki ni jambo la hiyari katika misingi ya demokrasia.
Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Uwanja wa ndani wa Makao Mkuu ya CCM Kisiwanduwi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Alisema Uchaguzi Mkuu wa marudio Zanzibar hakuitishwa na CCM, CUF au Chadema, bali Tume ya Uchaguzi ndiyo walioitisha baada ya kujiridhisha kuwa Uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ulikuwa na kasoro.
Alisema mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec)ndiyo yenye mamlaka ya kuratibu na kusimamia uchaguzi Zanzibar.
“CCM tumeshakubali kushiriki uchaguzi wa marudio na suala la kushiriki au kutokushiriki ni jambo la hiyari katika demokrasia,”alisema Dk. Shein.
Alisema uchaguzi wa Zanzibar umelazimika kurudiwa ili kukidhi matakwa ya demokrasia na kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kukamilisha haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha, Dk. Shein aliwataka wananchi kudumisha na kuimarisha amani ya Zanzibar lakini alionya serikali haitofumbia mtu yeyote ambaye atajaribu kuvuruga amani na mshikamano kwa wananchi wake.
Alisema vyombo vya dola vipo makini kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarishwa na kuwataka wananchi kuendeleza utamaduni wa Zanzibar wa kuiishi katika mazingira ya amani kwa manufaa ya Zanzibar na watu wake.
Alisema kurejewa kwa uchaguzi Zanzibar isiwe sababu ya kuchafua amani ya nchi na kuonya kuwa kwa mwenye ubavu ajaribu kufanya na kwamba atakiona cha moto.
Dk. Shein alisema uchaguzi utafanyika kwa amani na salama na kwamba sio kweli kama kutakuwa na sitofahamu kama inavyodaiwa na watu na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Upande wake mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema wana-CCM wasibabaike na kauli ya CUF ya kutoshiriki uchaguzi wa marudio wa Machi 20, mwaka huu.
Acheni kulazimisha nyie; mnataka watu wauwane tuu; kuweni wastaarabu
ReplyDeleteacha udikteta wewe watakuua udikteta wako wote utaenda kuufanyia makaburini we ropoka tu.!
ReplyDeleteKATIKA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA 2010 KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR DR.SHEIN ALIPATA ASILIMIA 50.1 NA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ALIPATA ASILIMIA 49.1 HII YOTE BAADA YA FIGISI-FIGISU TA ZEC,LEO HII SHEIN UNAMDHIHAKI MAALIM KIASI HICHO? MWENYEZI MUNGU YUPO PAMOJA NA WANAODHULUMIWA.
ReplyDeleteAma kweli kwenye siasa hakuna mungu watu wanaonekana wacha mungu kumbe walafi tu madaraka yan hata hofu awana me naona kama ndo ivyo kusiwepo na kampen tena znz ccm wajitangazie ushind maisha yaendelee
ReplyDeletedah
ReplyDeleteubabe ako utapambana na Mungu inshallah
ReplyDeleteCCM wasenge
ReplyDeleteTunawachukia kama hitler
Lakini dawa ipo jikoni