Mdee amesema kuwa kila ufisadi uliofanyika viongozi wa serikali walikuwa wakitambua sababu kuna muda mwingine walipokea memo kutoka katika uongozi wa juu ya nchi.
Halima Mdee amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Kawe na kusema kuna wakati wakurugenzi walikuwa wanapewa vimemo kutoka kwa Rais wa nchi na wengine walikuwa wakipewa memo hizo kutoka kwa mawaziri mbalimbali.
"Hakuna ufisadi ambao umefanyika kwa bahati mbaya, hakuna ufisadi ambao umefanyika nchi hii pasipo waziri au aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi kujui. Hakuna ufisadi uliofanyika leo hii bila wakurugenzi kupewa vimemo ama kutoka kwa Rais, au kutoka kwa waziri wafanye maamuzi waliyofanya leo wanajifanya wanatumbua vijipu kumbe wanatumbua vipele, sababu wale walifanya kwa maelekezo ya wakubwa." Alisema Halima Mdee.
Katika hatua nyingine mbunge huyo wa Kawe amesema kuwa wao wanapozungumza leo hawazungumzi tu kwa sababu ya Chadema na UKAWA bali wanazungumza kwa maslahi mapana ya watanzania walio wengi ambao maisha yao ni magumu yaani kifupi wamepigika.
Huyu nae nini Halima anarudia matapishi tulishachoka na kiki zenu za kijinga hayo yalishapita na zama zake kweli walikuwa hawashughulikiwi mafisadi mpaka mkamlea top la mafisadi kwasasa mafisadi wanashughulikiwa kisawasa kwa vitendo na tunaona kwa hao anaowasema kama anaushahidi apeleka mahakamani sio kutuletea longalonga hamna jipya
ReplyDeleteunaongea nn wewe bila hawa kina Mdee na UKAWA hawa mafisadi wangekuwa wanatamba tu, ccm isingewastopisha hao.
DeleteSi-chadema si-ukawa mmeishiwa, hamna jipya, fungeni 'mabakuli yenu'. Hivi lile FISADI PAPA lenu 'kwamfano' lingeshinda uraisi, ungethubutu kusema hayo makorokocho yako?? Au ndio maneno ya mkosaji mpfyuuuh, mtu mzima hovyoooo. Bila haya wala aibu mmelipigia debe FISADI PAPA mkaambulia patupu, sasa hivi unapozungumzia mafisadi ujue na Lowasa 'presidaa wenu' anahusika..........FUNGA BAKULI LAKO
ReplyDelete