Mwakyembe na Halima Mdee |
Mdee aliibua tena suala la kashfa ya ununuzi wa mabehewa hayo 274 akisisitiza kuwa ni mabovu, wakati alipopata nafasi ya kuchangia katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2011/- 2015/16 ambapo aligusia ahadi ya serikali ya kukarabati reli ya kati ambayo alidai haijatekelezwa ipasavyo.
Dk. Mwakyembe alikanusha taarifa ya kuwepo kwa mabehewa mabovu kati ya mabehewa hayo 274 yaliyonunuliwa wakati akiwa Waziri wa Uchukuzi.
“Leo nikimwambia Halima aniletee mabehewa ambayo hayafanyi kazi atashindwa kunionesha,” alisema Mwakembe
Waziri huyo alieleza kuwa mkataba wa ununuzi wa mabehewa hayo ulitoa mwanya wa kufanya ukarabati au marekebisho katika bidhaa husika ndani ya muda fulani, kipengele kinachojulikana kama ‘defect liability period’.
Hivyo, alitumia kipengele hicho kufanyia marekebisho mabehewa hayo ambayo alikiri hayakuwa mazuri yalipowasilishwa.
“Mabehewa yote yanafanya kazi kwa sababu yalipoletwa ni mimi mwenyewe nilisema kuna mabehewa ambayo sio mazuri. Nikaunda uchunguzi, kwa sababu tulikuwa na haki chini ya mkataba (defects liability period), ilikuwa ndani ya mwaka mmoja, wakaja wale walioutuuzia mabehewa wakayatengeneza. Sasa yako wapi hayo mabovu?” alieleza Mwakyembe.
Juzi, Mwakyembe alieleza kuwa yuko tayari kujiuzulu ubunge wake kama itabainika kuwa madai ya kashfa hiyo ni ya kweli.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge wa upinzani walitaka ripoti ya uchunguzi wa ununuzi wa mabehewa hayo iwasilishwe bungeni huku wakisisitiza kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria ya ununuzi iliyopelekea ununuzi wa mabehewa mabovu.
Anao
ReplyDeleteCCM mna matatizo gani wewe kumwita Halima mwanafunzi wako bungeni ina husunini kwetu ni mbunge tena kwenye eneo lako
ReplyDeleteFyuuu mwakembye
hivi unawezaje kununua kitu kibovu ili ukakitengeneze au alitengeneza kwa gharama zake. acheni ufala, huyo mbaba ni fisadi. ustafu ubunge wakati ubunge wenyewe umeupata kimagumashi.
ReplyDeleteHUNA JIPYA MSENGE WEWE LABDA BABA YAKO NDIYO FISADI
DeleteSenge wewe
DeleteUfisadi wa nchi hii unaanzia kwenye familia. utakuta mtu yupo mbali anatafuta maisha akituma pesa ya maendeleo kwao lakini ndugu wanazitafuna
ReplyDeleteHalima Mdee Fisad Papa pia njoo Bweni utajua,,,nyie si mnasema tu kwa vile mashabiki kama team ya mpira,,,
ReplyDeleteFunga domo wewe
Delete