Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya, amevuliwa wadhifa huo kwa madai ya kuchelewa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Amani Mwenegoha.
Utekelezaji wa kumvua madaraka mwalimu huyo, Mathias Mazuri, ulifanywa na Ofisa Elimu Shule za Msingi wa wilaya hiyo, Shadrack Kabanga.
Mwalimu Mazuri alichelewa kikao kilichoitishwa na Mwenegoha Februari 6, kikiwa na lengo la kudhibiti fedha za ruzuku ya Serikali na kwamba adhabu hiyo ni fundisho kwa watumishi wengine.
Akitangaza kumvua wadhifa huo mbele ya walimu wakuu wenzake, Kabanga alisema Shule ya Butinzya ipo karibu na eneo la mkutano na wezake waliotoka mbali walifika saa 3:00 asubuhi yeye saa 6:00 mchana.
“Sikubali, huu ni muda wa kubadilika siyo kuleana, nakuvua wadhifa kuanzia sasa siyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya,” alisema.
Mwalimu Mazuri alijitetea kuwa kuchelewa kwake kulitokana na pikipiki yake kuharibika njiani, utetezi huo ulitupiliwa mbali na ofisa elimu.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mwenegoha aliwataka walimu kutumia vizuri fedha za ruzuku na kwamba, wasichangishe wazazi kutokana na uhaba wa posho za madaraka.
Mwenegoha alipiga marufuku kuwadai wanafunzi fedha za masomo ya ziada.
Sasa hii sifa,
ReplyDeleteEnter your comment...upuuzi mtupuu
ReplyDelete