Jaji Lubuva Amshukia Edward Lowassa Kwa Anavyojitangaza Kuwa Alishinda Urais na Jina Lake Kukatwa


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu waache kujitangaza kuwa walishinda, akisema wanapotosha wananchi.


Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya aliyekuwa

mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kudai kuwa kama si matokeo kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.


Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari ofisini kwake, akisema yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.


Jana, akiwa kwenye mkutano wa tathmini kati ya NEC na asasi za kiraia kuhusu utoaji elimu kwa mpigakura uliofanyika Dodoma, Jaji Lubuva alisema uchaguzi umeshapita na kilichobaki sasa ni kufanya kazi tu.


Bila ya kutaja jina la mwanasiasa huyo, Jaji Lubuva alisema kama kuna mtu alishindwa katika uchaguzi uliopita, ajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.


“Hata wananchi wanawashangaa kwa kuwa wao ndio walioamua ni nani anafaa kuwaongoza,” alisema Jaji Lubuva.


Alisema kuwa NEC ilikuwa inapokea matokeo ya uchaguzi kutoka majimboni na kuyasoma kama yalivyotumwa na katika hilo hakuna wakala hata mmoja wa chama ambaye aliyapinga matokeo hayo.


“Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa.


"Sasa kama kila atakayeshindwa atataka tume ifukuzwe kazi hapatakuwa na tume ya uchaguzi kwa sababu kila atakayekuwa anashindwa atakuwa anataka tume ifukuzwe kazi,” alisema Jaji Lubuva.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wakati mwingine kukaa kimya kunasaidia,ifikie wakati tuache kumuongelea Lowasa maana ni sawa na kupiga gitaa kwa mbuzi.Kushindwa kashindwa,Mungu mwenyewe katuchagulia JPJM ingawa kwa macho ya binadamu tulijidanganya Lowasa ndio angekuwa rais,wasimamizi wa kimataifa wamesema uchaguzi ulikuwa wa haki.Imekuwa kawaida kwa UKAWA kulalamika kuibiwa kura,na Lowasa ni mpinzani hivyo ataendelea kulalamika tu,dawa ni kuachana nae.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili nalo neno.Na uchaguzi 2020 atashindwa vibaya sana.

      Delete
  2. Huyu mzee lowassa nae ni JIPU.waziri anaehusika kwenye utumbuaji wa majipu ya aina hii embu wajibika hapo...Ametushaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad