Jaji Mihayo Afunguka Kuhusu Wanaosema Rais Magufuli ni Dikteta.....


Mwenyekiti wa Majaji wastaafu, Jaji Mihayo amesema Rais Magufuli sio dikteta kwani hajafanya lolote linalomfanya awe juu ya sheria.

Amesema “Wanaosema Magufuli ni dikteta hawawajui madikteta. Hakuna kiongozi dikteta Afrika Mashariki isipokuwa Idi Amin tu,” Jaji Mihayo, ambaye ni mwenyekiti wa majaji wastaafu, alihoji inawezekanaje kiongozi ambaye mataifa mengine wanatamani akaongoze nchi yao angalau kwa miezi miwili, aonekane kuwa ni dikteta. “Magufuli anafuata sheria kwa sababu hajafanya jambo lolote ambalo linamfanya awe juu ya sheria. Sijawahi kusikia kasema mfunge huyu au kusema sheria hii isitumike na hii itumike” alisema.

Alisema ni kawaida kwa viongozi wanaokemea uovu kuonekana kama madikteta kwa sababu wanataka kuondoa rushwa.

Kadhalika, Jaji Mihayo alisema anaupenda utendaji kazi wa Magufuli ili wanaokiuka sheria wawajibishwe na walalahoi wapate haki yao.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli wanaompinga Ni mafisadi gari kumi ,Na watoto Wao wanasoma ulaya ,matibabu ulaya haya yamekwisha wote tuwajibike kuijenga nchi kwa pamoja sio masikinu tuu Na walala hoi

    ReplyDelete
  2. Dah!yaani!Mungu akuongee umri Jaji Mihayo,watu kama nyie ndio mnaojua haki na naamini ndio nyie mliosemwa na Magufuli ya kuwa mnastaafu bila kujilimbikizia mali.Hivi Magufuli unamuitaje dicteta wakati hata hao ambao wana kesi zilizo wazi anasema sheria ifuatwe?si angeamuru tu adhabu fulani kwa kutumia rungu lake.Eeeh!aliyeturoga watanzania sijui nani jamani,Mungu ambariki Magufuli wetu.

    ReplyDelete
  3. Tunahitaji sala tu,maana wanaompinga magufuli ni wengi sana.
    Mungu amuepushe na hila zao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad