Jeshi la Kenya KDF limethibitisha kuwa limemuua kiongozi wa al-shabab anayesimamia intelijensia ya kundi hilo Mohammed Karatey pamoja na makamanda wengine 10.
KDF limesema kuwa liliwaua wapiganaji hao katika shambulio kubwa mnmo mnamo tarehe 8 mwezi Februari.
Kulingana na taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na wizara ya Ulinzi nchini Kenya,wapiganaji hao waliuawa katika kambi ya Nadaris kati ya Buale na Sukow.
Inadaiwa kuwa Karatey alikuwa amezuru kambi hiyo kwa hafla ya kufuzu kwa takriban wapiganaji 80 wapya wa alamnyat waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi.Inadaiwa kuwa wapiganaji 42 waliuawa huku wengine wengi wakipata majeraha.
Kitengo cha alamnyat ndicho chenye wapiganaji wa kujitolea muhanga,wataalamu wa vilipuzi na watafutaji habari hivyobasi mauji ya kamanda huyo ni pigo kubwa wa alshabab.