Kauli ya Magufuli ya Kwamba Ataendelea Kufanya Kazi Aliyotumwa na CCM Yazua Utata..Wadau Wadai Atengue Kauli

Kauli aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli, ya kwamba ataendelea kufanya walichomtuma chama cha CCM, imeibua mtafaruku miongoni mwa wananchi huku wakidai amewasaliti.

Wakitoa maoni yao katika ukurasa wa Facebook wa East Africa Television wananchi hao wamesema kauli hiyo ya Rais Magufuli haikuwa sahihi, na wengine kumtaka atengue kauli yake kwani walimchagua kama Magufuli na sio chama.

"Hahahaaa ni kweli katumwa na CCM na ndo wamempa mbinu zote za maigizo na scripts zote... sijapendezwa sana Rais wangu kwa kauli hiyo.... Atengue kauli please!! Wengine tulichagua yeye kama Magufuli ila sio yeye kama mgombea wa ccm... I hate CCM and all members wa hicho chama... Kama na yeye yuko kichama zaidi, hatutavutiwa naye pia”, alisema Revocatus Obote.
Mdau mwengine aliendelea na maoni haya...

“Ameshabadlisha kauli yake tayari,

ni kazi ambayo ametumwa na CCM sio wananchi tena, sasa kama ni kweli anataka kufanya kazi aliyotumwa na ccm inamaanisha kuja kumalizia pale alipoacha huyo wa Chalinze, kuja kuimalizia nchi yenyewe sasa”, alisema Kannole Kaisy.

Mdau mwengine alisema kutokana na kauli imeonyesha ni tatizo la kuchagua viongozi ambao sio vijana, na kushauri kuwapa nafasi vijana ili kupata fursa ya kuliongoza Taifa, ikiwemo na kubadili katiba ya nchi.

“Aseee yani hii nchi inaendeshwa kichama sio, kwahiyo CCM ndo anaiongoza na sio wananchi wa Tanzania, hili ndo tatizo la kuchagua wasio vijana siku hizi, kuna low expentance sasa hii katiba inabidi ibadilishwe ili vijana wapate fursa za kugombea urais, unajua sisi atuendelei kutokana kila secta unakuta mzee ndo anaongoza, tuwaige wenzetu basi yani Tanzania kila kitu bàdo tuko nyuma, dah yani bora kuzamia ulaya tu kwa mambo kama haya, we bado ufikilie jinsi ya upatikanaji wa ajira kwa vijana na mambo mengine ya nchi unaongoza chama sasa we unadhani na mtafaruku unao endelea nchini we unadhani vijana hawatojiunga kwenye makundi ya ajabu”, alisema mdau aliyejulikana kwa jina la Cannibal Man.

Jana kwenye sherehe za kutimiza miaka 39 chama cha mapinduzi (CCM), Rais Magufuli alisema ataendelea kufanya kazi aliyoagizwa na CCM, kauli ambayo imeleta minong'ono mingi miongoni mwa Watanzania.
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnashangaa nini sasa, yeye amegombea uraisi kupitia ccm na anaongoza nchi kwa kutekeleza sera za ccm. Na kila chama kilichogombea kilikuwa na sera zake hivyo chama chochote ambacho kingeshinda kinyume na ccm kingeongoza kwa kutekeleza sera za chama husika.

    hata akichaguliwa kijana bado atatelekeza sera za chama alichotoka acheni kukuza mambo

    ReplyDelete
  2. Kikwete alishaimaliza nchi kwa kubarikiwa kichama. Chama kimeiteka nchi. Wanachama wa ngazi za juu wote Wa Tanzania wamepeana maslahi makubwa yote ya nchi hii. Tumeanza kumwona Mkapa, Kikwete wakitumia usemi kimafumbo eti wapo tayari kufanya kazi na Magufuli. Pia wanawaomba Wazee wawe karibu. Hapa Kikwete moja kwa moja amejisafisha mwenyewe kwa kujiweka karibu na Magufuli kusudi Magufuli ashindwe kumzatiti Kikwete kwa kuharibu nchi. Mabadiliko wanayoyataka Watanzania, na waliyoyataka Watanzania si haya.Tuliwaambia Watanzania wengi walioipigia CCM ya kuwa mtu mmoja hawezi kubadilisha nchi, Mfumo wa CCM ni uozo. Ne wajanja wanaofanya kila njia kutokupelekwa mahakamani kwa wizi, ufisadi mkuu, udanganyifu, mauaji yasiyo na vielezo. Majumba na miji inayojengwa bila vielezo, ardhi walizopeana, mabiashara,Ukitaka uwe tajiri haraka ingia CCM kubali wizi utakuwa bilionea. Sheria, na Wanasheria hawapo huru. Wanasheria wengi wamepewa na kuwa ndani ya mfumo hata kumpata mwanasheria safi ni ngumu. Sababu hata yeye yumo kwenye mfumo wa CCM. Chukua chako mapema. Watajifungaje wenyewe? Wala Mkapa pia haaminiki. Ni chini ya uongozi wake viwanda vilitaifishwa na mabenki, majumba na migodi wakagawiana na kwenda ubia na watu wa mataifa ya nje kuwaibia Wananchi wa Tanzania. Mnashauriwa na mataifa makubwa kuuingia ubepari na ukabaila kwa manufaa yao kwa kukejeli Watanzania na kuwaibia Watanzania. Wanastahili kufunguliwa kesi za jinai hawa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naona umeandika mengi sana.Hivi ni chama kipi Tanzania ambacho wewe unadhani kinaweza kuubadili huo mfumo? Chadema ya Mbowe na Lowasa? Au CUF ya Seif ?

      Delete
  3. CCM NI WALEWALE ILA KAENI MTAMBUE KWAMBA KUNA WATU WALISEMA KUWA MBIO HIZO ZITAISHIA SAKAFUNI.HAHAHA POMBE MAGUFULI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo ni dua za kuku,mpaka sasa hakuna mbadala wa CCM Tanzania. Integrity ya viongozi wa upinzani ni questionable.

      Delete
  4. CCM wasenge Na nyinyi mliyo pigiakura wasenge

    ReplyDelete
  5. sijiu kina Obote na wenzio achane siasa za kijinga mnageuka kama kinyonga kukidhi haja zenu za kimasilahi hamuitaki CCM wala magufuli mnakaa mnaropoka kama machizi

    ReplyDelete
  6. Hapo cha ajabu ni nini?Magufuli alipigiwa kura akiwa ni mgombea wa CCM na ilani iliyotumika katika kampeni niya CCM,na yeye yupo kutekeleza ilani hiyo.Hutaki,hama..

    ReplyDelete
  7. Mbona kiswahili safi katumia,nashangaa watu mnatoa mapovu.CCM ndio waliompendekeze kugombea urais,na katiba anatumia ya CCM,lakini ni rais wa wote kwa kutumwa na CCM kututumikia.

    ReplyDelete
  8. NDIYO!KATUMWA NA CCM,KWANI KATUMWA NA CHADEMA?

    ReplyDelete
  9. UPINZANIIII MNAPANIKIIIII SANAAA MBONA MMECHAGUA WAZIRI VIVULI BUNGENI KAMA MNAMTAMBUA RAISI SI MKE BAKI A MAWAZIRI WAKEEE CCM WATAWABURUZA SANAAAAAAAAAAAAA TUUUUUUU

    ReplyDelete
  10. Watu wanapenda kukuza mambo jaman ..mzee si ni mgombea kutoka ccm na pale ikumbukwe alikuwa kwenye maadhimisho ya ccm ...sasa nyie wapinzani na akili zenu za kuku mlitaka ahubiri nn pale!!!mtu anaongea kwa mujibu wa mazingira aliyopo na hata ile cku ya maadhimisho ya mahakama aliongea according to mazingira na maada husika na kuna kitu aliongea utafikiri alikuwa anajua ...akasema watasema ameingilia mahakama....kweli asubuhi yake kwenye udaku wakaandika magufuli aingilia mahakama...kumbe yeye anaongea anachostahili kuongea lkn mabongo lala yanaanza kutapika fyuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad