Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.
Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mia mbili.
Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;
1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.
2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.
3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.
4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.
5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??
Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;
Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.
(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;
Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.
Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.
Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.
Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.
Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.
Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.
Nawasilisha by Stroke/Jamii Forums
Kauli ya Rais Imevunja Katiba; kwa Kuingilia Uhuru wa Mahakama
14
February 05, 2016
Tags
Kwani vikorokocho mnakosekana?
ReplyDeleteJipangeni tu kumkosoa Magufuli lakini mkae mkijua Mungu yuko juu yake na anampa ulinzi wa kutosha,kwa kuwa hafanyi wala hakei uhalifu kwa ajili ya tumbo lake tu bali ni kwa manufaa ya wananchi wote.Na nina uhakika wewe ni mmoja kati ya hao wenye kesi 400.Kama mtu umekutwa na nyara mkononi,ushahidi wa nini?au kwa nini kwenye kutafuta ushahidi iwe zaidi ya miaka 5....?
WW jifanye mchambuzi Tu, Hilo jipu lako la kwenye mat...!!!litatumbuliwa Tu ,naona ndio wachawi WA nchi hii,hata ukisema Ni dikteta ,ndio rais sasa kaamua WW utaishia kuandika Tu.
ReplyDeletePOLE SANA WIVU NDO SIFA YENU ULITAKA ASEME NINI NAWE UWE NA FURAHA
ReplyDeleteWatanzania mnapenda mfanyiwe nn? sasa kama ushahidi upo...documents zipo ...watu walikwepa kodi, y serikali isishinde kesi zote?? inafikia wakat lazima tuache siasa tuitangulize tanzania mbele wote kwa maslah ya wote na sio maslah ya kisiasa, ni kiongozi gani ambae mnamtaka aendeshee hii nchi....kutoka mbinguni au?
ReplyDeleteHata wenzetu wanaoendelea wanabana matumizi sio kutumia tuu sababu zipo tuna mambo mengi ya kufanya Na muhimu mno sio kila kitu mnakandia Go Go Mr President tulipanga foleni ndefu kukuchagua wewe
ReplyDeleteGo go Mr President yupo nyuma yk wala usiogope tulishazoea lazy lazy kila SK mgonjwa kz hakuna sasa kumekucha bana matumizi kila sehemu Na hapa kazi ndio tutafika
ReplyDeleteNa mambo ya kuahirisha kesi hapo mengi utasaga vumbi yangu asubuhi mpaka saa Tisa jaji hayupo kwenda kwenye kikao ,makaratasi hayaonekani faili limefungiwa,hayo yote majipu Na yanajuana sasa kumekucha
ReplyDeleteMnanishangaza watu mnaojifanya wataalam wa Katiba katika kutetea maovu. Kweli mmezoea uvundo, hamtaki tena kusafishiwa zizi.
ReplyDeleteKama wewe ni mtaalam wa Katiba, tuoneshe kifungu kinachomruhusu mtu kutolipa kodi ya serikali kwa miaka mitano na zaidi...au tuoneshe kifungu kinachomhalalisha afisa TRA kumiliki nyumba 73 na rundo la magari ambayo hata hatumii... Unakuna kichwa? Bado nimekukalia kooni; tuoneshe katika Katiba yako toleo la nyumbani kwenu kifungu kinachompa jangili mamlaka ya kutungua Chopa...
Kama huna majibu wewe ni jpu la sehemu za nyeti, utumbuliwe mchana kweupe na kadamnasi ya wazalendo. Hufai kitu ng'o.
Ata sijui umeongea nini...hiyo hiyo katiba inamruhusu rahisi kutoa uamuzi wa mwisho so ndo kaamua sasa ata kama serikari azitoshinda kesi zote bali itasave ela kidogo ......Go magufuli fanya kazi baba kama umemkuta mtu na ushahidi unataka uendelee kuchunguza nn sasa hapo...
ReplyDeleteWakukaya kazi tu hapa
ReplyDeleteMajaji wengi ni matapeli wana tabia ya kusoma kesi kwa kiingereza ili kutisha watu
Wengi hata kiingereza hawakijui vizuri
Fukuza fukuza wote
kwa maudhui ya uandishi na elimu yangu ya falsafa robo tatu ya maoni yaliyotolewa ni ya mtu mmoja,bwana au bibi go-go,go.asiguswe mheshimiwa rais,asikosolewe aa.yeye anawalenga liberals kisha kuwashambulia kama hivi alivyoonyesha katika maoni yake.ni mpuuzi wa kweli.kilichosemwa ni cha weledi wa taaluma ya sheria na wanasheria.ni moja ya nguzo kuu za utawala bora,ni moja ya misingi imara ya kidemokrasi.suala la mahakimu na majaji kutenda haki,kuhukumu kwa kufuata sheria tuu linatakiwa lisimame hivyo milele.haki nasema haki ndio ufunguo wa ustawi wa nchi kama taifa na uhuru kamili chini ya jua.mheshimiwa rais alizungumzia mengi tena ya maana sana mfano kucheleweshwa kesi bila sababu za msingi,wote tunaunga mkono kwa nguvu zote.lakini hili la kui-quantify mahakama ,kuiweka kama sehemu ya TRA ya kukusanya maduhuri inapaswa kukataliwa na walengwa yaani mahakimu na majaji,vinginevyo katika mahakama zetu yatafuguliwa matawi madogo ya benki kama zilivyo ofisi za tra .kesi za madai zote faini[uliona wapi],tumepewa lengo la kukusanya shilingi trillion moja ili tuweze kama mahakama, kupewa motisha nono.huu sio utawala bora.
ReplyDeleteDubai Magufuli kutakuumbuwa peleka matumizi
ReplyDeletehuyu mwandishi fala kweli, ndo majipu haya!
ReplyDeleteMpimeni
ReplyDeleteSamaki WA Magufuli yallichia wapi