Kesi Ya Kafulila Yahirishwa Mpaka March 9, 2016 Baada Ya Mawakili Wa Serikali Kutofika Mahakamani Leo

KESI No. 2 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma kusini iliyofunguliwa na mlalamikaji  David Kafulila dhidi ya mbunge Hasna Mwilima,Msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa serikali imeahirishwa leo na mahakama kuu kanda ya Tabora mpaka  marchi 9, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa tena.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa  ianze mapema leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma,  Mbele ya Jaji Dr Wambari ambae pia ni Mkuu wa chuo cha sheria lushoto mkoani Tanga, imeahirishwa kwasababu mshatakiwa Hasna pamoja na wakili wake Kennedy Fungamtama pamoja na mawikili wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo, kwa madai ya kuchelewa kupata wito wa mahakama hiyo, huku mlalamikaji David Kafulila akifika na wakili wake Prof Safari.

Katika mazingira hayo Jaji Wambari aliagiza mawasiliano yafanyike kwa pande hizo ili kujua ni lini kwa hakika mawakili hao wataweza kushiriki katika kesi hiyo.

Kutokufika kwa mlalamikiwa  na mawakili wake na wale wa upande wa serikali ilipelekea zoezi la kusikiliza kesi hiyo kusimama kwa saa mbili kutoka saa tano asubuhi  mpaka saa saba mchana na baada ya hapo hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Jaji silivesta Kahinda alisema  kuwa kesi itaendelea march 9 mwaka huu na kwamba kwakuwa tarehe hiyo imependekezwa na mawakili na pande zote mbili.

Akiongea na mtandao huu mlalamikaji wa kesi hiyo David Kafulila alisema kuwa anakubaliana na uamuzi wa mahakama hivyo aliwataka wananchi wawe na subiri hadi hiyi tarehe 9 march mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad