Kikwete Kuwatumbua MAJIPU Wanachama Wasaliti wa CCM Waliokihujumu Chama Wakati wa Uchaguzi Mkuu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amesema kuwa chama chake kitawachambua na kuwaadhibu wote ambao walikisaliti katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo Jumatatu ya wiki hii mjini Kibaha alipohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi mpya ya chama hicho mjini humo.

“Baada ya mchakato wa Dodoma wapo ambao walisusa kabisa na wakawa wanajificha. Unakuta hahudhurii mikutano yetu ya kampeni, lakini ya wenzetu upinzani unamkuta na akiulizwa anasema eti alialikwa,” alisema na kusisitiza kuwa wanachama kama hao ni wasaliti na uanachama wao una mashaka.

Kikwete alisema mchakato wa kuwaadhibu wanachama wasaliti utafanyika wakati wowote baada ya kuyapitia majina ya wote wanaotuhumiwa kukihujumu chama.

“Tayari tuna majina ya watu ambayo yanadhaniwa walikihujumu chama. Tutayapembua katika vikao mbalimbali halali kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa na Taifa na tutaamua kwa haki wakati wa kuwaadhibu,” alisema.

Aliwataka wanachama hao kufanya tathmini na kutambua waliokisaliti chama lakini alionya vikao vya kuwabaini vitende haki bila kumuonea mtu akisema yapo baadhi ya majina yanatajwa kuwa ni wasaliti kutokana na migogoro binafsi baina yao.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unafiki mtupu,ulikuwa wapi siku zote?wadanganye hao hao?

    ReplyDelete
  2. mnafiki sana huyu jamaa, tumekuchoka kaendelee na anasa zako ulaya

    ReplyDelete
  3. unakumbuka shuka, kumekucha

    ReplyDelete
  4. Mungu atatulipia tu sisi watanzania wenzako jinsi ulivyotufanyia katika miaka 10 ya urais wako fake

    ReplyDelete
  5. AENDEE AKAFANYE UZINZ KWINGINE TANZANIA TUSHAMCHOKA KWANZA ANATAKIWA KUFUKUZWA TANZANIA AMEKULA NCHI NA WANAE SANA.

    ReplyDelete
  6. AKITUMBUA WENZAKE NA WENZAKE WATAMTUMBUA KWANI SI WANAYAJUA YA KWAKE ALIYOYAFANYA KATIKA TAIFA LAKE, ALIKUWA WALA HALITAKII MEMA, BALI UZANDIKI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad