KIMENUKA..Zari Hassan Mpenzi wa Diamond Atajwa Kuwa ni Mwanachama wa Freemanson Uganda

Mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameorodheshwa kwenye listi ya watu maarufu nchini Uganda ambao ni wanachama wa jamii ya siri ya Freemason kisa kikielezwa kuwa ni utajiri alionao wenye maswali mengi.

Habari kutoka Kampala, Uganda zilizoripotiwa hivi karibuni zilieleza kwamba, mwanamama huyo ana ukaribu mkubwa na matajiri wa Nigeria ambao wanaaminika kuwa utajiri wao ulitokana na kuwa ‘memba’ wa mtandao huo mkubwa duniani.

Ilidaiwa kwamba, Zari amekuwa akifanya kufuru ya fedha zinazowashangaza wengi, kuwa kwa muziki au biashara gani anazofanya zinazomuingizia mkwanja mrefu kiasi cha kumiliki magari ya kifahari kama Lamborghini na Hummer ambayo yote ameyaandika majina yake badala ya namba za usajili.

Katika habari hiyo, wengine waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa mumewe aliyezaa naye watoto watatu, Ivan Semwanga, wachungaji maarufu nchini humo na wanamuziki kama Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ na Bebe Cool.


Zari anayemiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala nchini Uganda, anasemekana kumiliki vyuo vya urembo na maduka ya vipodozi nchini Afrika Kusini huku akijiingizia mkwanja kupitia shoo zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya.

Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Zari hakupatikana badala yake aliyezungumzia ishu hiyo ni mpenzi wake, Diamond ambaye alisema kuwa mama mtoto wake ana miradi mingi na siyo kama wanawake wa mjini ambao wanabweteka badala ya kutafuta mkwanja.

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HIYO MIRADI ANAIJUIA ILIKOANZIA? HUYU HANITHI AKAMSAIDIE BABA YAKE KWANZA

    ReplyDelete
  2. shangazi anamiradi ya Ivan sasa Dai anajitapa hajui chanzo wala wisho. endelea baba ushakuwa ndondocha wa ug.

    ReplyDelete
  3. sasa inawahusu nin nyie si ni maisha yake kajichagulia....ikumbukwe kuwa kila mtu anaishi kwa imani yake wewe kama unaamini utafanikiwa au umefanikiwa kupitia njia flan aidha ni kanisa/msikiti au uganga ni wewe na yeye wepesi aliuona uko huko anakoamini......watu sijui wakoje kila kitu muandike ...F*OFF

    ReplyDelete
  4. Ivi watu wanafikiri utajiri unakuja kilelemama eeeeh......uliza matajiri wote unaowafaham watakwambia wamepitia wapi na wapi mpaka wakafika hapo walipo

    ReplyDelete
  5. jamani kwani uwezi kucomment kwa lugha nzuri...mpaka matusi

    ReplyDelete
  6. Leo anaduka la vipodozi kesho anahoteli kubwa,wee haya wee yetu macho...wapi Daudi kanyau kwenye misaada yote kwa jamii kumbe anadili zake but good luck girl

    ReplyDelete
  7. neno tajiri ni tamu sana kulitamka. na hasa ukimtaka kumpa kiki mtu.

    ReplyDelete
  8. Hatuhusu sisi hata wanachama WA boko haramu

    ReplyDelete
  9. sasa km anajulikana vitu anavyofanya na kumuingizia pesa maduka mahoteli sasa kinachowashangaza ni kitu gani kaanza kidogo kidogo mpaka kafika pakubwa kwani bakhresa na wengine wameanzaje ndo mana hatuendelei mana tumekalia majungu mtu hujiulizi ufanye vp ili umfikie unakalia kuwaza freemason kila mwenye pesa ni freemason imani zenu mbaya ndo zinawapotosha na dini ya mtu ni imani ya mtu so ww unaamini freemason ndo mana ukakubali kwamba utajiri wake unatokana na freemason ingia na ww upate hela buuu shit

    ReplyDelete
  10. tajiri au muuza nyapu uyo. acheni kumpaisha bi kizee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. na wew kauze au sinunuliki mwenzetu?
      fyuuuuuuu

      Delete
  11. Mtakufa masikini badala ya kutia bidii mpate vyenu mnakalia kuwasema walionavyo hata hivyo mpanda ngazi na mshuka ngazi hawashikani mikpno

    ReplyDelete
  12. mbona Dai hamuoi? si alikuwa anataka demu tajiri ili asimpe pesa zake.

    ReplyDelete
  13. ivan anauza madawa ya kulevya,kila mtu anajua uganda na kundi lao,kuhusu zari kuwa freemason sina hakika ila diamond ni freemason

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad