Kundi la Wanamgambo wa Kiislam ISIS Lamkata Kichwa Kijana Baada ya Kumkuta Akisikiliza Nyimbo zenye Mahadhi ya Marekani

KUNDI la wapiganaji la ISIS limemuua kwa kumkata kichwa kijana mmoja baada ya kumkuta akisikiliza muziki wa Pop unaoimbwa na wasanii wa Marekani akiwa kwenye baa ya baba yake.

Kijana huyo, Ayham Hussein (15) alikamatwa mjini Mosul, Iraq baada ya wapiganaji waliokuwa kwenye doria kumsikia akisikiliza muziki huo.

Mauaji hayo yalifanyika nje ya msikiti baada ya Hussein kutiwa hatiani na mwili wake umekabidhiwa kwa wazazi wake kwa taratibu za mazishi.

Mbali na kuuawa Hussein, vijana wengine wawili nao wameuawa kwa kupigwa risasi nje ya msikiti kwa kutohudhuria Swala ya Ijumaa.

ISIS walipiga marufuku miziki ya nchi za magharibi kupigwa kwenye maeneo yao huku sababu kuu ikitajwa kuwa miziki hiyo ni chanzo cha vitendo viovu, majaribu pamoja na kumfanya mtu kushindwa kujifunza Koran hivyo kumsahau Mungu.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dooh!!yaani kuna baa pia kwenye maeneo yao!..kama ni matendo maovu mbona wanayafanya wao? Sijui ni mungu gani hawa jamaa wanaabudu!!!!

    ReplyDelete
  2. Roho imeniuma jamani km mwanangu?? Huu ukatili watauacha lini hawa watu?? Tunapoelekea Ni vita ya tatu ya dunia kati ya wakisto Na waislam. Ehee Mungu tunusuru waja wako!!

    ReplyDelete
  3. Hii iman gani jamani. Mungu kweli ndio atakavyo hivi

    ReplyDelete
  4. Wao huyo mungu wao ni yupi alie toa Mari ya kuwachinja wenzao kama kuku na kitabu kipi kinasema hivyo wamelaaniwa kabisa

    ReplyDelete
  5. Wamewaua wakristo zamu yao kuuwana wenyewe kwa wenyewe

    ReplyDelete
  6. kinachoendelea sasa hivi ni propaganda hilo kundi la ISISI linadhaminiwa na marekani kuwaangamiza waislam wa Syria na IRAQ , kwa mtazamo katika dini ya uislam hakuna amri inayosema kuuwa nafsi ya mtu, ni katika madhambi makubwa yasiyo sameheka mbele ya mungu, na km dini hii ya uislam ingepelekwa hivi km inavyofanywa na haya makundi ya sasa, basi huu uislam usingetufikia, mtume muhammad aliepotea hii dini na ikasambaa ulimwengu mzima bila kufanya mauaji, kuongoza watu katika dini inahitaji hikma

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad