Lowassa na Mbowe Nao Wanashinda Maskani..Dudu Dudubaya Afunguka..Story Kamili iko Hapa

Dudubaya amesema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alipokuwa akiwaelezea watu aina za maskani zilizopo na kusema kuwa zipo maskani zingine ni mbovu kwa kuwa zibapoteza watu na kuharibu watu na kudai kuwa zipo maskani zingine ni endelevu kwani watu wanabadilishana mawazo kuhusu mambo fulani na kusaidiana mawazo pia.

Dudubaya amewachana baadhi ya mashabiki ambao kupitia kipindi cha eNEWS walisema kuwa Dudubaya saizi amepoteza njia na muda mwingi amekuwa ni mtu wa kushinda vijiweni, ndipo hapo aliposema kuwa mashabiki hao kwanza ni wanafiki na mamluki, ambao wanalengo la kutaka kumchafua adai ni watu wasiomjua vizuri ambao wametumwa.

"Hao mashabiki ni mamluki tena ni kenge tu hao na mimi nitaendelea kuwa mamba, hawa jamaa hawajui maana ya maskani wanapaswa kuelewa kuna maskani potofu ambazo watu hawakuwa machangudoa lakini wanafundishwa na wanakuwa machangudoa, kuna maskani ambazo watu wanafundishana wizi, lakini wanapaswa kutambua zipo maskani zingine ni endelevu watu mnasaidiana na kubadilishana mawazo kutokana na fani zao hata kina Lowassa na Mbowe wana maskani zao, wanamichezo wana maskani zao hata sisi wanamuziki wana maskani hata idea za ngoma zangu zote zinatoka maskani, muziki wa Juma Nature unatoka maskani, hivyo sitaacha kukaa maskani ili mradi maskani yangu ya watu timamu ambao wanajua majukumu yao, lakini pia wanapaswa kutambua mimi sishindi kijiweni toka asubuhi mpaka jioni nakwenda maskani jioni baada ya kumaliza mishe zangu." Alisema Dudubaya.

Dudubaya aliongezea na kusema msanii kuwa kimya si kigezo cha kufulia kwani wengine wanatumia muda huo kwenda shule kufanya mambo mengine ya msingi au wengine wapo kwenye biashara zao, hivyo msanii kukaa kimya haina maana kuwa amefulia.

"Saizi kama unavyoona King Crazy GK yupo kimya kwa muda kwenye game lakini juzi juzi hapa amemaliza chuo na sasa ana Masters yake yupo kimya kimuziki sababu kuna jambo alikuwa anafanya la msingi, na kama unavyojua mashabiki zetu hawa wanasema kila siku kuwa wasanii wa Tanzania hawana elimu, lakini tena ukifanya maamuzi hayo labda kurudi shule wanasema umefulia sijui wanataka nini mashabiki hawa" Alisema Dudubaya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad