Lubuva : Rais Magufuli Hana Mamlaka yoyote ya Kuingilia Uchaguzi wa Zanzibar Kama Watu Wanavyotaka

Mwenyekitu wa Tume ya Uchaguzi alikutana na Rais Magufulu jana na Amebainisha kuwa wanaosema Rais anapaswa kuingilia kati masuala ya uchaguzi iwe Tanzania bara ama Zanzibar wanafanya makosa, kwani kwa namna yoyote Rais hana mamlaka hayo na hivyo hawezi kuingilia maamuzi ya tume hizo

“Unaposikia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano aingilie hilo suala la uchaguzi wa Zanzibar, yeye kwa kweli hana mamlaka kabisa. Pili ni kama kujikanganya, huku unasema tuwe na tume huru isiyoingiliwa halafu huku unasema aingilie kati maamuzi ya tume” alisema Jaji Lubuva.

Jaji Lubuva amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikatiba hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar na hata huku bara pia hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume.

Mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi amewasihi watanzania kuwa uchaguzi umekwisha, na kuwaomba waungane na viongozi waliochaguliwa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo.

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MANENO YA AIBU KUBWA,YANAYOOGOFYA NA KUSIKITISHA SANA TOKA KWA JAJI MSTAAFU,MWANATAALUMA WA SHERIA NA MWENYEKITI WA KUTEULIWA NA MHESHIMIWA RAIS, WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI.ANASEMA 'RAIS HANA MAMLAKA'NDANI YA TANZANIA YETU.NIMEINGIWA NA WASIWASI MKUBWA NA UTIMAMU WA SASA WA AKILI ZA JAJI MSTAAFU.NI VIZURI SASA AKAPIMA AFYA YAKE YA AKILI MIREMBE.RAIS NI AMIRI JESHI MKUU NA NDIYE TANZANIA ONE KWA LOLOTE LINALOHUSU TANZANIA NA RAIA WAKE KWA MAAMUZI AIDHA KWA KUSHAURIWA AU KWA KUTOKUSHAURIWA HUSUSANI AKIONA NCHI INAYUMBA KWA JEURI YA TAMAA MBAYA.ZANZIBAR NI TAMAA MBAYA.

    ReplyDelete
  2. BUuuuulllSHiiiit !!!!!!!!!!!!!1

    ReplyDelete
  3. Basi asipeleke majeshi Zanzibar

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad