Lundenga Asikitishwa na Maneno Yanayosambazwa Mtandaoni Kuhusu Hoyce Temu...

Hashim Lundenga
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (pichani) amezungumza  kuhusu habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kumhusu Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu.
Lundenga amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania na Mtanzania wa kawaida amesikitishwa na maneno hayo na kuwa hayapendezi kusemwa kwa mtu kama Hoyce ambaye amejitoa kusaidia jamii.
Alisema kuwa anashangazwa na mtu ambaye amekuwa akiandika maneno hayo mtandaoni kwani hawakuwa na utofauti wowote na kilichokifanya ni kumuandika Hoyce ambaye hakuhusika katika ugomvi uliokuwepo baina ya mtu huyo na mdogo wake Hoyce, Rachel.
“Nimesikia habari hizo kumhusu Hoyce kwa kweli nimesikitishwa sana, sio jambo zuri ambalo amelifanya huyo aliyemuandika,” alisema Lundenga.
Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka watumiaji wa mtandao kuwa na matumizi mazuri ya mtandao ili kuzidi kuifanya mitandao ya kijamii kuwa sehemu salama kwa ndugu na marafiki kuwasiliana.
Zaidi unaweza kusikiliza maneno ya Lundenga hapa chini.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mange aliyekubuhu duniani hadi akhera WA kugombana naye
    Angalia hata mashoga zake bongo kila kukicha kuzuia scandali
    Naona hata kisha data

    ReplyDelete
  2. MCHEPUKO WAKO AU NDIO SHEMEJI, MAANA UNAOAGA MAMISS.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad