Maalim Seif Sharif Hamad Amshushia Tuhuma Nzito Jakaya Kikwete..Adai Yeye Ndio Amevuruga Uchaguzi wa Zanzibar

Katibu Mkuu wa (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa madai mazito kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana yalipinduliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha, baada ya kupata baraka za Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Alisema, saa chache kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutangaza kufuta uchaguzi huo, kituo kikuu cha kutangazia matokeo kilichokuweko Hoteli ya Bwawani kilizingirwa na vikosi vya jeshi na polisi na kwamba kitendo hicho kuwa ni “Mapinduzi ya Kikatiba”.

“Aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati ule alikuwa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na ndiye aliyepeleka vikosi vile baada ya kuona chama chake kimeelekea kushindwa kwa upande wa Zanzibar,” alisema Maalim Seif na kuongeza;
“Dkt. Shein wala Balozi Seif (Seif Ali Idd) hawamiliki jeshi wala polisi, vile ni vikosi vya Dk. Kikwete wakati ule na hawezi kukwepa lawama ya kuingilia uchaguzi wa Zanzibar.”

Maalim Seif pia amewashutumu baadhi ya viongozi wakiwemo wa dini wanaojaribu kupotosha ukweli na kuunga mkono uamuzi batili wa kurejewa uchaguzi uliotangazwa na ZEC.

Unaichukuliaje kauli hii ya Maalim Seif?

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kelele za chura hazimfanyi tembo hasinywe maji!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mnadharau Demokrasia kwa kujifanya kelele za chura. kuna siku mtajua kwamba haki ya mtu haipotei bure.Ubabe una mwisho na uonevu pia. Kumbukeni kuna Mungu.

      Delete
    2. Mungu ndio amepanga uchaguzi urudiwe zanzibar

      Delete
  2. Anamaslahi binafsi kupitia wawekezaji ndio wanaomtunukia heshima kimatafa bandia katumika sana wakati wa uongozi wake. Hushangai anasifika kuleta amani nchi nyingine akiacha kidondandugu kwake. Mwenye akili asingethubutu kupokea hivi visifa akijua wazi nchi yake inachezewa. Mwache achezewe na mataifa makubwa yenye maslahi nchini. Naye siku ya kutumbuliwa yaja na mwanae na mkewe.hawawezi kulikwepa hili.

    ReplyDelete
  3. Anamaslahi binafsi kupitia wawekezaji ndio wanaomtunukia heshima kimatafa bandia katumika sana wakati wa uongozi wake. Hushangai anasifika kuleta amani nchi nyingine akiacha kidondandugu kwake. Mwenye akili asingethubutu kupokea hivi visifa akijua wazi nchi yake inachezewa. Mwache achezewe na mataifa makubwa yenye maslahi nchini. Naye siku ya kutumbuliwa yaja na mwanae na mkewe.hawawezi kulikwepa hili.

    ReplyDelete
  4. haki wapi nyie haki mbinguni kwendeni ukoo
    hatuongozwi na machotara sisi

    ReplyDelete
  5. JAMBO HILI LILIKWISHA ELEWEKA MAPEMA TOKA TAREHE 27 OCTOBA`2015.VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA KUJUA MATOKEO YA CHAGUZI YEYOTE INACHUKUA SIKU MBILI TUU.DR.SHEIN ALIMWARIFU KIKWETE KWAMBA AMESHINDWA VIBAYA NA SEIF SHARIFF HAMAD NA KIKWETE AKAMJIBU KWAMBA CCM KAMWE HAITOSHINDWA UCHAGUZI.HAPO NDIPO ZILIPOUNDWA NJAMA ZA KUMTUMIA JECHA 'KUUFUTA UCHAGUZI WOTE'ZANZIBAR.ULIKUWA NI UAMUZI WA KIDIKTETA,MKUU KASEMA NA NDIPO ZANZIBAR ILIPOTUMBUKIZWA KWENYE ULINZI WA KIJESHI KILA UPANDE,KILA KONA KUHAKIKISHA TANGAZO LILE LA KIHALIFU LA JECHA LINASIMAMA.ANAYEIWEKA NCHI YETU MAJARIBUNI KWA SASA NI KIKWETE AMBAYE BADO NI MWENYEKITI WA CCM.ILIELEKEA WAKATI FULANI MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI ALIKUA AMEUTAMBUA UKWELI LAKINI MAGUFULI BADO HANA SAUTI CCM.KILIITISHWA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM,MHE.RAIS MAGUFULI ALIALIKWA KAMA MWALIKWA MAALUM NA KIKAO KILE KIKAPITISHA AZIMIO ZITO LA KUIUNGA MKONO CCM ZANZIBAR,KUENDELEA KUMTAMBUA SHEIN NA KUAPA KUYAENZI 'MAPINDUZI MATUKUFU'YA ZANZIBAR.KUANZIA HAPO MHESHIMIWA MAGUFULI AKASALIMU AMRI.HAPO MHESHIMIWA RAIS AKANAWA MIKONO.KIKWETE ANAENDELEA KUTAMBA KWA KOFIA YA UENYEKITI WA CCM,MAGUFULI AKIWA MWANACHAMA WA KAWAIDA WA CCM.HILI NI TATIZO KUBWA LA TANZANIA YA LEO,CCM.NAWAAMBIENI KAMA AMBAVYO KAMPENI MENEJA WA MAGUFULI ABDALLAH BULEMBO ALIVYOWAHI KUONGEA HADHARANI WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU OCTOBA 2015 HUKO MWANZA NA BUKOBA "CCM ITAITAWALA TANZANIA MILELE".NDIZO CHECHE HIZI TUNAZOZIONA. KWA UPANDE WA CCM UHALALI HAKUNA,NI UBABE,UDIKTETA,WIZI,VYOTE KUTOKA CCM YA LEO,CCM YA KIKWETE ANAYEIANGAMIZA ZANZIBAR SASA.

    ReplyDelete
  6. watu sijui wana matatzo gani? Wamejaaliwa kweli kuropoka

    ReplyDelete
  7. Baadhi wanataka kujiunga na Gbagbo The Hague ama vipiiii?

    ReplyDelete
  8. SISI CHURA EEE,ASANTE CCM.MNAENDELEA KUTUDHARAU,KUTUDHIHAKI KWA SABABU MMEIKAMATA DOLA.DOLA NI CCM NA CCM NI DOLA.MUNGU YUPO.UWEZO WETU,NGUVU ZETU,MAAJABU YETU VYOTE VITATOKA KWA MUNGU,WAKATI HUO UTAKAPOKUA UMEFIKA WAKATI HUO KWENU NYINYI CCM, UTAKUA NI WAKATI WA KUSINYAA,KUPARAGANYIKA,KUSAMBARATIKA NA WENGI WENU KUISHIA KWENYE MAGEREZA.MHALIFU SIKU ZAKE 40 TUU.HAIZIDI,HUU NDIO MPANGO WA MUNGU.

    ReplyDelete
  9. Chura MAMAKO mbuzi weeee

    ReplyDelete
  10. Africa ni maskini sababu viongozi wengi wakiwamo maraisi ni vibaraka.
    Ni lini Mwafrika ataamka.
    Ni lini Waafrika watatumiwa na Wakoloni hupitia uchumi wetu, mabanki, mikataba na mbinu mataifa makubwa yanapanga kila siku kuwatetea maraisi mbumbumbu wasio na elimu.
    Kwa nini shweria za Afrika haziwekewwi maanani.
    Kwa nini Maraisi wanaogopwa hata tukijua ni wezi na mafisadi.Kwa nini uhuru unanyimwa. Kwa nini Wanajeshi wasomi wa ngazi za juu wanatumika na maraisi waovu.
    Kwa nini polisi pia wanatumika.Na sasa hata hawa polisi wakuu wanakesi mara tu wanapotoka.
    Kwa nini familia za Wakuu zinaogopwa. Na wengi wao wanakokotwa kwenye siasa hata sifa hawana. Kwa mfumo huu wamejazana kila secta, kila ofisi wanakula, wanafilisi, wanalagai na kutamba.
    Kwa nini wasiachishwe kazi wanaposhikwa na tuhuma.
    Je Tanzania kama ndi hivi, Magufuli atayaweza? Je Kuna Wanaccm madarakani wanaomuunga mkono na kumsaidia, Kwa nini Magufuli asiwateue Wapinzani Watendakazi na wenye uchungu wa nchi hii?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad