Maandamano ya Vijana wa CHADEMA Kwenda Ikulu Kushinikiza TBC Ionyeshe Bunge LIVE Yapigwa Marufuku

Jeshi la Polisi kanda Maalumu Dar, limepiga marufuku maandamano ya Vijana wa CHADEMA kwenda Ikulu kwa lengo la kushinikiza TBC ionyeshe Bunge LIVE.

Kamanda Sirro amesema kuwa hakuna taarifa na pia hakuna uthibitisho kuwa maandamano hayo yatapokewa na Rais Magufuli.

Pia, Kamanda Sirro alieleza kuwa BAVICHA hawakuanisha barabara ambazo wanatarajia kutumia katika maandamano hayo.
 “Siku hiyo sio nzuri sana kwa sababu ni siku ambayo watu wanakuwa kazini. Ni siku ambayo wengi watataka kutumia barabara hizo kwa ajili ya huduma za kijamii. Na kwa sababu kuna option nyingine ya kuweza kupata suluhu hiyo, nisema tu kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku,” alisema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad