MAMLUKI waliobaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku zao zinahesabika, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, kumuagiza Makamu Mwenyekiti, Tanzania Bara, Philip Mangula kuanza kuwashughulikia.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Namfua, mkoani Singida, Kikwete alisema chama hicho kimevuka salama katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba mwaka jana, pamoja na baadhi ya wenzao kuondoka.
“Tunashukuru uchaguzi ulipita na Chama kimevuka salama katika mchakato mzito kinyume na watu walivyotutabiria kifo… haukuwa rahisi kwetu kwa sababu ulizidiwa na kelele na vitisho pamoja na kuwepo wenzetu waliotuhama na kudhani tutakufa lakini hatukutetereka.
“Tunajua wako wengine waliobaki kama mamluki, lakini wajue siku zao zinahesabika maana hatutakubali kuendelea kunyonywa damu, natumaini Mangula umeanza kuwashughulikia hawa mamluki,” alisema Mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake.
haya sasa mzee wa mipasho, rais mtalii mstaafu uliyemwachia jembe wetu jpombe kazi kubwa ya kurudisha mamilioni uliyoyateketeza wewe ndiye mamluki namba one na siku zako zimeisha kaa pembeni acha tingatinga awe huru.
ReplyDeleteHahaaa yepp... the kenge has spoken. Umpe ruhusa na halfani amtembelee baba yake nguza angalau mara moja kwa mwezi....
ReplyDeleteMakubwa
ReplyDeletemzushi kaa pembeni tuachie pombe wetu asafishe uozo ulioacha
ReplyDeletemzushi kaa pembeni tuachie pombe wetu asafishe uozo ulioacha
ReplyDeleteNdo maana Singida tulikataa kukupa mke hufai
ReplyDelete