Matikibokoyao: Wema Sepetu Rudisha Pesa za Nguo Unazodaiwa na Manyota

Aliyekuwa shabiki namba moja wa muigizaji wema sepetu(Team wema) , matilda au maarufu kama matikibokoyao ametoboa moja ya siri ya aliyekua boss wake kuwa huwa anakopa nguo kwa mfanyabiashara maarufu mjini aitwaye manyota, hivyo amemtaka msanii huyo mpenda kick mjini aende akalipe madeni ya watu.

Akiendelea kumwaga ubuyu, Yuda huyo hakumuacha nyuma muigizaji lulu michael na kudai kuwa na yeye pia ana madeni sugu kama ilivyo kwa boss wake(Wema).

Chanzo cha bifu hicho inasemekana ni mimba aliyokua nayo staa huyo(wema) ambapo inadaiwa mfuasi wake huyo nambari moja amekua akitembeza ubuyu kwa maadui zake(wema) kuhusu ujauzito wake ambapo boss huyo aliamua kumchana live kijakazi wake huyo na kumkana hadharani kuwa hamjui.

Bifu hilo liliendelea mbele zaidi ambapo shabiki huyo wa madame aliapa kutoboa siri kibao za boss wake huyo , hata hivyo baadae madame baada ya kuona mambo yake yanaanza kuanikwa alianza kujirudi taratibu kwa mfuasi wake huyo na kuyamaliza kiutu uzima

Chanzo: Jamii Forums

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. masikini matiti kibogoyo ndio nani tena? labda ndio wale wanaotaka kujulikana kwenye magazeti kupitia watu fulani! mtu awe na gari ashindwe kununua nguo wewe matitiboro sio vizuri kha

    ReplyDelete
  2. Umaa arufu kazi kweli hamlali bila wema,,,Bank zeneyewe zinadaiwa itakuwa wema,,,,acheni umburula chapa ilale

    ReplyDelete
  3. wazungu dunia nzima hawatumii cash wanatumia credit card kukopa ni mfumo au system ya maisha serikali yetu ni tajiri inaingiza bilions ila tena inakopa na kusaidiwa acheni ushamba wema yuko juu kwa kila kitu her english acsent is perfect body yake sauti yake the height yani wema ni mzuri for everything ana kasoro za kibinadam but yuko sawa lov you wema

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad