Matokeo ya Uchaguzi wa Raisi Uganda...Huyu Ndio Rahisi wa Uganda Aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi hii.
MUSEVENI

Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.

Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.

Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad