Mh Mbowe |
Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Mwananchi na kueleza yafuatayo:
“Hatujawahi kama kambi ya upinzani kumtenga Zitto kwenye kila jambo, yapo mambo tunaweza kulazimika kutengeneza ushirikiano na wabunge hata wa CCM ili kufanya jambo fulani kutekelezeka.
“Kushirikiana na Zitto si jambo la ajabu kama ambavyo umeona tukilifanya. Yapo majeraha mengi ambayo tumeyapitia pande zote (CHADEMA na Zitto) ambayo huwezi kuyatibu kwa siku moja. Yapo ambayo yatapona kulingana na muda. Unaweza kumfanyia mtu kitu kibaya, lakini baadaye ukatambua kuwa umekosea. Chochote katika siasa kinawezekana,” alisema Mbowe.
Zitto alifukuzwa Chadema na kujiunga na ACT Wazalendo Machi 21, 2015 chama ambacho hakina ushirikiano na vyama vinavyounda Ukawa lakini katika siku za karibuni ameonekana kuwa karibu na umoja huo wa wananchi, ikiwa ni pamoja na kushirikiana kuibua hoja mbalimbali katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Source: Mwananchi