Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu '
Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai
Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.
Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .
Kwa nini Serikali ya Tanzania imeshindwa kuwaelimisha Watanzania namna ya kutii na kutumia sheria. Inakurupuka kila siku kwenye matukio kama haya sababu imeshindwa kutoa elimu mbadala vijijini na kuwachukulia wavunja sheria hao. Si vijijini tu makazini hata Wasomi hawajui sheria za nchi. Kwa muda wa miaka hii kumi kumezidi mauaji ya kinyama, madawa ya kulevya, ufisadi. Viongozi wako kwenye wizi na hawafuati sheria. Hata wanasheria wapo busy kuvunja sheria. Nchi imekuwa ikijiendesha kienyeji sababu viongozi wote wakuu wako kwenye biashara zao za horere. Ni watu wa mitaani wasio na sifa za uongozi. Hata tunapozungumzia haya hawaelewi sababu hawana ustaarabu kabisa wala haya. Ni watu waliotoka kwenye mazingira ya uswahilini. Vurugu vurugu tu.hadhi kwenye misamiati ya kwao haipo.
ReplyDelete