Mfuko wa Habari Tanzania (TMF ) Wasema Uko Tayari Kutoa Msaada wa Fedha Ili Kuiwezesha TBC Kutangaza LIVE Mwenendo wa Bunge

Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko  wa  Habari Tanzania (TMF) Ernest Sungura amesema taasisi yake iko tayari kugharamia matangazo ya  live Bungeni  kupitia TBC  ili  kuwawezesha  wananchi  kujua  kinachoendelea  Bungeni.

Akizungumza leo jijini  Dar  es  Salaam katika mkutano na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari nchini mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari( MAELEZO), Assah Mwambene, Sungura  amesema lengo la TMF ni kuleta mabadiliko chanya  katika tasnia ya habari na kuona wananchi wanapata taarifa kwa wakati.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie watu, kama mnazo pesa za kuchezea, hebu jengeni madarasa mnunue na madawati, hilo bunge la 'mipasho','misutano','taarifa', 'miongozo' hakuna ulazima wa kuliona 'live', hata likirekodiwa inatosha, na tutayasoma magazetini......wabunge wengi 'wasema-hovyo' wanatafuta 'kick', waonekane ni mahodari wa 'kubwabwaja' na kuuza sura zao.......TUMESTUKA, HATUTAKI BUNGE LIVE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga, huyo Mkurugenzi ameamua mwenyewe kufanya hivyo, kama kweli wewe unauchungu na maendeleo ya nchi mbona haujawakosoa wanaotumia fedha kwenye maazimisho ya vyama vyao?

      Delete
  2. Sungura gani usiyea na akili uchangie mambo ya mipasho kama ya taarabu bungeni na watu kila kukicha wanatoka bungeni vurugu zisizoisha nini cha maana kitatusaidia ni bora kama huo mchango wako ungeupeleka sehemu ziko kibao tanzania kusaidia jamii wenye shida leo unajitia kifua mbele kutafuta misifa

    ReplyDelete
  3. Ndg zangu kama kupata habari ni haki ya kila mtu kwa nini ninyi wachangiaji mwanze kuleta utata? waliojitolea acha atoe wapo wanaoguswa kwenye madarasa akina Mengi pia kwenye barabara sio kila mtu ataguswa kwenye kipaombele chako. unavyofikiri sio wote wanafikiri hivyo. Mbona marais waliopita waliwaza tofauti na huyu aliyepo sasa? ameona tofauti ameanza na nidham ninampa hongera tena safi sana, na hawa TMF acha wachangie tupo tunaotaka kuangalia.

    ReplyDelete
  4. pelekeni hizo pesa sehemu zenye shida kama elimu, madawa au jengeni zahanati

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad