Mgogoro wa Wamasai na Wamang’ati Wamalizwa Wilayani Kondoa

Juhudi za viongozi wa serikali wanasiasa na viongozi wa mila kutoka mikoa ya Manyara na Dodoma wakiongozwa na naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi William Ole Nasha wamefanikiwa kumaliza mapigano ya watu wa jamii ya kifugaji kutoka makabilia ya Masai na Mang'ati (Tatoga) waliyokuwa wanagombania Ng'ombe na kusababisha vifo vya watu wawili katika mpaka wa wilaya za Kondoa na Simanjiro.

Kikao hicho kilichofanyika kwa zaidi ya masaa tisa viongozi hao wakiongozwa na naibu waziri Ole Nasha iliwabidi kutumia busara kubwa kumaliza mgogoro huo ambapo kabla ya muafaka hali ilikuwa hivi.

Baada ya kikao viongozi wa kisiasa kutoka katika kabila hizo mbili mbunge wa Simaniro James Milya mbunge wa Hanang Mary Nagu Flatei Maasai wa Mbulu vijijini na mwenyekiti wa halmashauri ya Simanjiro Jackson Sipitek wakatoa kauli zao.

Baadae naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi William Ole Nasha aliongoza muafaka huo akaitimisha kwa kueleza walicho afikiana hadi kufikia makubaliono ya kusitisha mapigano hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad