Mrembo na Mwigizaji Thea Adaiwa Kuhongwa Gari

STAA wa filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ sasa hivi anasukuma mkoko baada ya kutembea kwenye vumbi kwa muda mrefu lakini pia taarifa zilizo nyuma ya pazia zinadai eti kahongwa na mwanaume.

Inadaiwa baada ya Thea kumwagana na Michael Sangu, alijiweka kwa mwanaume mwenye nazo na ndiye aliyempa jeuri ya kumiliki gari hilo aina ya Toyota Passo.

“Thea sasa mambo safi, anatembelea makalio baada ya kuhongwa gari na yule bwana wake wa sasa,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kunyaka ‘ubuyu’ huo, Thea alitafutwa, alipopatikana alisema: “Hili gari sijahongwa na katika maisha yangu sitegemei kuhongwa na mtu yeyote, nimenunua kwa hela yangu ninayopata kwenye muvi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kila mtu ana malengo yake,Kama kununua gari angeweza kununua siku nyingi,lakini tu Thea alikuwa anafanya vitu vingine, kamaliza sasa kanunua gari.Na ikumbukwe hawa wametoka kupewa mkwanja na CCM.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad