Mtanzania anayesoma India amepigwa, kuvuliwa nguo na kisha kulazimishwa kutembea akiwa uchi na kundi la watu nchini humo.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21 (jina linahifadhiwa) anayesoma shahada ya biashara, mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore, alifanyiwa ukatili huo akiwa na Watanzania wengine wanne.
Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore, liliripoti kuwa tukio hilo lilitokea Januari 31, baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa India, mkazi wa Hesaraghatta aliyekuwa na mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.
Nusu saa baadaye, Watanzania watano akiwamo aliyevuliwa nguo, walifika katika eneo hilo wakiwa kwenye gari ndipo kundi la watu hao lilipoanza kumshambulia binti huyo, kisha kumvua nguo na kumlazimisha atembee uchi.
Baada ya kuchoma gari lililosababisha ajali hiyo, kundi hilo pia liliteketeza gari alilokuwamo Mtanzania huyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga alisema Balozi wa Tanzania nchini humo, John Kijazi ameshakutana na wanafunzi hao na ameshazungumza na Serikali ya India kuhusu tukio hilo.
Gazeti la Deccan Chronical liliripoti kuwa licha ya polisi waliokuwapo eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote hata pale msamaria mwema aliyejitokeza kumsitiri msichana huyo kwa fulana yake ambaye pia alipigwa huku fulana hiyo ikichanwa.
Mshauri wa masuala ya sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika wanaosoma Bangalore, Bosco Kaweesi alinukuliwa na gazeti la The Chronical akisema hata dereva wa gari alilokuwa Mtanzania huyo, Micah Pundugu alipigwa na kujeruhiwa vibaya.
Alisema hata pale msichana huyo alipojaribu kupanda basi ili kujinusuru na zahama hiyo, abiria walimshusha.
Msichana Mtanzania Anayesoma India Amepigwa, Kuvuliwa Nguo na Kisha Kulazimishwa Kutembea Akiwa uchi
10
February 04, 2016
Tags
Dah! pole sn ila ninacho fahamu mm wahindi kwa kiasi flani ni wabaguzi hasa kwa watu wenye ngozi nyeusi sijajua kama wana roho mbaya kiasi cha kumdhalilisha mtu kisa ni mwafrika.......
ReplyDeleteSERIKALI IKEMEE HILI NA IMESEME IMECHUKUA HATUA GANI?
ReplyDeleteKweli selikali iliangalie ili kwa macho yote mbili, dada yetu pole sanaa
ReplyDeleteWao wakija nchi za kiafriks km Tanzania wanaonekana km waungu ndio maana wanafanya hivyo Ni nyoko Sana hawa watu..adui wabaguzi mno shenzi hawafai kabisa fyuuu
ReplyDeleteWahindi siyo watu wazuri hata kidogo hasa kwa watu weusi wewe angalia hata hapa walioajiriwa kwa wahidi wakikueleza wanavyo nyanyasika utachoka lakini sisi tuna wakumbatia ukisema unaambiwa ubaguzi
ReplyDeleteSijajua serikali ya Tanzania imesema nini juu ya hii,hali hii ni mbaya kuliko.
ReplyDeleteSerikari itasema nn? Sabab nayo inanyenyekea kwaajili kufankisha mambo flan, ss mm au ww tutapga kelele sana mwsho wa sku huwezi ata kuskia chembe ya habar juu ya hatua zlizochukuliwa zid ya watu waliofanya unyama huo.
ReplyDeletekudadeki zao wahindi ...hawa watu wabaguzi sana na wana roho mbaya kishenzi...pole dada yetu .....yaani nawachukia nataman ata wangefukuzwa tu Tz.NK
ReplyDeleteUbaguzi upo kila kona ya dunia ulaya'america na asia hata africa jambo la maana ni balozi zetu zielimishe wanafunzi watanzania wanaoenda nje ya nchi,na sheria za kuwabana wanaowanyanyasa cha kufanya ni balozi zetu kushirikiana na watanzania ktk nchi zenye wanafunzi kutoka nyumbani kwakuwa wanajua mengi kuhusu hizo nchi.
ReplyDeleteUbaguzi upo kila kona ya dunia ulaya'america na asia hata africa jambo la maana ni balozi zetu zielimishe wanafunzi watanzania wanaoenda nje ya nchi,na sheria za kuwabana wanaowanyanyasa cha kufanya ni balozi zetu kushirikiana na watanzania ktk nchi zenye wanafunzi kutoka nyumbani kwakuwa wanajua mengi kuhusu hizo nchi.
ReplyDelete