Mwakyembe: Katiba Mpya sio Kipaumbele cha Rais Magufuli....Wanaofikiri Tutaanza Na Rasimu Ya Warioba Wanapoteza Muda

Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria amewataka Watanzania wanaoulizia hatima ya mchakato wa katiba mpya kutambua kuwa suala hilo si sehemu ya vipaumbele vya Dk. John Magufuli.

Mwakyembe amesema hayo jana usiku katika mahojiano maalum aliyofanya na Marin Hassan, mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), juu ya utendaji wa wizara yake katika siku 100 za serikali ya awamu ya tano.

Waziri huyo alisema kuwa katiba mpya haina umuhimu mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu na wala sio kipaumbele cha rais Magufuli kwani ni kiporo tu alichoachiwa na serikali ya awamu ya nne na atakifanyia kazi wakati atakapoona inafaa.

“Watu wanadhani katiba mpya ndiyo kila kitu, wanaona katiba ni muhimu kuliko kulipia watoto waende shule, wanafikiri katiba mpya ikishapitishwa tu basi kesho yake wataletewa mkate na chai kitandani jambo ambalo sio kweli,” amesema Dk. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa: “Kwa sasa rais bado anafanyia kazi vipaumbele vyake kwanza ikiwemo kusimamia elimu bure, kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya serikali na kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma na hivyo kelele za katiba mpya hazina msingi.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe alisema Watanzania ambao bado wana ndoto kuwa mchakato wa katiba mpya unaweza kuanzia katika hatua ya kujadiliwa kwa rasimu ya katiba ya Jaji Joseph Warioba kuachana na wazo hilo kwani limepitwa na wakati.

Alisisitiza kuwa katiba iliyopendekezwa na kupitishwa na wajumbe wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni halali kwani ilipatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu licha ya kususiwa na wajumbe wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Ukawa unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), National League for Demokracy (NLD) na NCCR Mageuzi.

“Rais alishasema alipohutubia bunge, kwamba kuna kiporo nimeachiwa, sasa mimi nashangaa hawa watu! tena wengine wana shahada za sheria, wanaongea nini? Hatua ya rasimu ya Warioba ilishapitwa na wakati na tayari tunayo katiba pendekezwa,” aling’aka.

Mwakyembe alihitimisha kwamba utakapofika wakati wa kulifanyia kazi suala la katiba mpya, serikali ya awamu ya tano itaendelea na hatua ya kura ya maoni ya katiba pendekezwa na sio vinginevyo.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Maendeleo ya wananchi kwanza. Elimu, afya, mapato, kazi halafu katiba baadaye.

    ReplyDelete
  2. Katiba pekee ndiyo itakayoweza kuwapeleka vigogo wanaolindwa na katiba ya sasa. Mnawaona wanahaha, na bado wanamtumia Magufuli. Maraisi waliopita walifanya juu chini kuipindisha katiba ili wasichukuliwe hatua kwani katiba ya zamani inawakinga hawa. Ni wao ndio inabidi watumbuliwe kwanza. Katiba ni mwongozo au kioo cha nchi. Bila kurekebisha Katiba huwezi kumshtaki Raisi aliyepita. Yeye ndiye chanzo cha haya yote ambayo Magufuli anayatumbua. Ni wao waliyalea na wao ni wahusika wakuu. Huwezi kutumbua vitoto ukaacha mzazi aliyeyasababisha haya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa akili zzako fupi unadhanii katiba unayoitaka ikipatikana marais waliopita watafungwa?
      jidanganye hvy hvy na akili zako za matakoni

      Delete
  3. katiba badae hakuna pesa za kulipa wajumbe wa bunge la katiba kwa sasa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad