Mwanasiasa Mkongwe, Augustine Mrema Atoa ya Moyoni Kuhusu Rais Magufuli Siku 100 za Ikulu...

Mwanasiasa Mkongwe, Augustine Mrema amemuelezea Rais John Magufuli kama kiongozi wa Tanzania anayetenda miujiza kutokana na utendaji wake ndani ya siku 100 tangu alipoingia madarakani.
Mrema ambaye alikuwa mbunge wa zamani jimbo la Vunjo na kuangushwa kwenye uchaguzi uliopita na James Mbatia (NCCR – Mageuzi), aliendelea kuutetea uamuzi wake wa kumpigia debe Dk. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ingawa chama chake cha TLP kilikuwa kimesimamisha mgombea urais.
“Nilijua wazi Rais Magufuli ni mtendaji ndio maana hata wananchi waliponiadhibu kwa sababu ya kumpigia debe sikuumia, najivunia chaguo langu na kiukweli anafanya miujiza ya hali ya juu,” alisema Mrema.
Mrema ambaye ni mwenyekiti wa TLP, alimuelezea Magufuli kama kiongozi mwenye uthubutu huku akiwataka watanzani kuacha unafiki na kumpa nafasi zaidi ya kufanya kazi

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huna mpango Mrema umemchoka kushinda CCM

    ReplyDelete
    Replies
    1. POVUUUUUUUUUU!KISA KAMSIFIA MAGUFULI?
      SOMENI TU NAMBA,HAKUNA NAMNA NYINGINE MAANA IMESHAKUWA NDIYO.

      Delete
    2. Ulitaka amsifie 'wakujinyea'???

      HAPA KAZI TU

      Delete
  2. Anasubiri apewe ukoo wa mkoa,hahaha haha,mrema jiuzulu nenda kanywe mbege.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad