Nape Nnauye Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Wa Habari Na Matukio Pamoja Na Meneja Wa Vipindi TBC

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bibi. Edna Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi.

“Tunachukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape

Aidha Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu.

Alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya watumishi wa Idara hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni  kujenga upya na kuboresha Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika lolote lile la Habari na kuongeza ufanisi.

Idara ya Habari na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri na Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na Meneja wa Vipindi wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na watumishi wengine watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Habari kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi hao.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa makosa yapi wewe Nape
    Msiige kila kitu mtapasuka misamba

    ReplyDelete
  2. It's fashion or reality
    Nakumbuka awamu ya pili naibu waziri WA elimu wakati huo
    Mayagila alimfukuza mkurugenzi wa elimu ya msingi kwa kasi hihi bila sababu za msingi
    Baadaye mayagila alijiuwa mwenyewe kwa risasi

    ReplyDelete
  3. Muwe mnafuatilia matukio mazee, wewe unadhani ile ishu ya kutangaza laivu sherehe za harusi kwa saa....ni jambo dogo? yawezekana pamoja na mengineo imechangia. Kamba hukatikia pabovu. Hayo ni mawazo yangu tu!.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Labda alipewa maagizo toka juuuuu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad