Nay wa Mitego Akimbilia Polisi..Achukua RB Adai Kuna Watu Wanamfuatilia Kutaka Kumtendea Mabaya

MKALI wa Bongo Fleva, ambaye wimbo wake wa ‘Shika Adabu Yako’ umefungiwa na Baraza la Sanaa Nchini (Basata), Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, ameibuka na kudai kwamba ameamua kuchukua R/B kituo kidogo cha polisi ili kuwadhibiti watu anaodai wanamfuatilia kwa nia ya kumtendea mabaya.

“Kiukweli sina ugomvi na mtu na hii ni dunia haina siri, kama kuna mtu ananifanyia hivyo vitu basi itajulikana maana mimi nimeimba kama wimbo mwingine na sina ugonvi nao, sasa kama wananitafuta nitawatafuta kwa R/B,” alieleza.

Aliongeza kwamba, kwa sasa mtoto wake wa kike amefanyiwa upasuaji wa uvimbe katika koo na maendeleo yake ni mazuri, huku akisisitiza kwamba Ijumaa ya wiki hii atatoa video ya wimbo wake huo.

“Mwanangu alikuwa anaumwa lakini kwa sasa nashukuru Mungu hajambo na wiki hii nitatoa video ya wimbo wangu, mtaona tofauti na mnavyofikiria tofauti katika wimbo wenyewe,’’ alimaliza


Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kawaida 'gang' huwa hakimbilii polisi,gang huwa nayamaliza mwenyewe iwe kwa shari au kwa kheri,huo wimbo wako wapo uliowagusia ukijua fika nao ni ma gang kukuzidi ww ss tulia,polisi ya nini na umeyataka mwenyewe?

    ReplyDelete
  2. we ndio uliwatusi wenzio so wenzio ndio wana haki ya kwenda polisi kukushitaki sasa wewe ndio umewawahi na kwenda polisi huoni hata hao polisi wanakushangaa na kukuona kilaza? kweli mtenda akitendwa huhisi kaonewa. mi wala sitashangaa likikukuta lolote wewe uwezi kuishi na wenzio kwa amani huna akili.

    ReplyDelete
  3. Hata uende wapi, kifiro kiko palepale, wewe si'unajifanya rijali bana?? Usiogope, subiri uvune ulichopanda

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad