Ni Ndoto Maalim Seif Kuwa Rais wa Zanzibar

Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama , Dr. Hassy Kitine ameweka wazi kuwa ni ndoto kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuiongoza Zanzibar.

"Watu wengi wanashabikia mgogoro wa Zanzibar bila kujua kiini chake, ili uzungumzie vizuri Zanzibar na harakati zake za kisiasa ni lazima uifahamu historia yake. Wenzetu wamepata uhuru wao kwa kumwaga damu, tofauti na sisi huku, ambako Mwalimu Nyerere alitumia meza ya mazungumzo kusaka uhuru, kwa wenzetu siyo" anasema Dr. Kitine.

"Bahati mbaya sana zipo siri zunazowagusa baadhi ya wataka urais wa sasa moja kwa moja, ambazo zinauhusiano mkubwa na Mapinduzi ya Zanzibar" Anaendelea kutanabahisha.

" Historia ya Zanzibar inawahusisha Waarabu(mabwana) na waswahili(watwana), hali hii iliendelea hadi pale Abeid Karume alipochukua uongozi wa visiwa hivyo na kuruhusu waswahili kuoana na waarabu ili kuondoa tofauti za kibwana na kitwana. Wapo watu wa ndni na nje ya nchi wanatamani mfumo wa kitwana na kibwana urudi visiwani humo na ndiyo maana wanahangaika huku na kule kutafuta uongozi, jambo ambalo haliwezekani kwa sababu nchi hiyo haikukomholewa kwa makaratasi" Dr. Kitine aliendelea kisema alipohojiwa na Rais nguvu ya Hoja.
"Hivi hamjiulizi ni kwanini Unguja hakuna shida, badala yake Pemba ndio kuonekane kugumu. Kuna historia nzito inayohusu usultani hapo Katikati, ambayo wengo hamuijui na hata wanaoijua jawapendi kuizungumzia" alisema.

"KITENDO CHA KUFUTA HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HAKIKUBALIKI NA HAKUNA MTU MAKINI ATAKAYEKUBALI KUFANYA HIVYO" Dr. Kitine alimazia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad