Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimuniufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.
Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa,itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?
Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.
Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
Picha ya Mwigulu Nchemba na Mwanae yazua Mjadala Mitandaoni
6
February 10, 2016
Mdau hata wewe ungekua Na uwezo ungempeleka mwanao Feza au zaidi ya hiyo ilo kila mtu anajua tatizo Ni Uwezo au pesa siyo cheo au uongozi big up Mr Mramba
ReplyDeleteSasa nyie mlifikiri atampeleka shule za kayumba?nyie endeleeni kukaraga bao bao na mtaisoma.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba shule za serikali hazina ubora ktk utoaji wa elimu kulinganisha na shule za binafsi kwasasa,makabwela tujiandae tu hapo baadae watoto wetu,wajukuu zetu kutumikishwa au kuongozwa na watoto waliotoka kwenye familia zenye kipato kikubwa walio soma shule za binafsi zinazo toa elimu bora
ReplyDeleteMtoa hoja hapo ni tatizo la uelewa. ukienda hotelini utakula chakula unachopenda, je shule binafsi ungependa nani akasome, mh na mtoto wake sio wabongo? hapo ametumia uhuru wake, mbona Nyerere alipenda watoto wake wasome hapa nchini ilikuwa chaguo lake. Tuache maneno tujadili vitu vyenye tija kama kukusanya kodi, kukamata watorosha twiga, mafuta baharini, na mengine mengi sio nani anasoma wapi au anakula nini.
ReplyDeletekwani tatizo liko wapi shule za binafsi ni kwa ajili ya wenyenazo na wapigiwa kura,.shule za kayumba au sirikali ni maalumu kwa wapiga kura wanainji makabwela au malofa aka mashabiki maandazi wa hapa kazi tu.
ReplyDeletemliupenda wenyewe na namba mtaisoma. hapa kazi tu na mbele kwa mbele
ReplyDelete