Polisi Dar Yakamata Magari 2 Yaliyotumika Kubeba Kompyuta Zilizoibwa Kwenye ofisi ya Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Philip Mpango.

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na komputa  na TV.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kutokana na oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.

Ameyataja magari hayo  kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CNV  na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV .Pia  walinzi wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo wamekamatwa.

"Katika wizi huo vitu vilivyoibwa ni Compyuta mbili, aina ya Dell pamoja na CPU, Monitor zake na Televisheni moja aina ya Sumsung inchi 40" Alisema Sirro.
Aidha kamanda huyo wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema katika oparesheni hiyo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 150 mali ya Bw Ahmed Huwel mkazi wa Msasani.

Katika hatua nyingine kamanda Sirro ametangaza kusitishwa kwa muda kwa shughuli za ulinzi shirikishi katika vituo vya polisi kutokana na vikundi hivyo kualamikiwa na wananchi kwa kutokuwa na tija katika jamii

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad