Baada ya kupitapita huku na kule katika maeneo yaliyotokea kadhia ya ujambazi jana nilifanikisha kunasa tukio Moja maeneo ya Chulwi Kongowe Mbagala kama sijakosea.
Mnamo 27.2.2016 majira ya SAA 12 jioni polisi walivamia harusi iliyokuwa ikifungwa msikitini na kuwakamata watu waliokuwemo ndani wakiwatuhumu kuhusika na Ujambazi uliofanywa siku ya tarehe 26.2.2016 katika tawi moja la Bank ya Access lililoko Mbagala.
Raia walisema polisi ilivamia msikiti na kuwakamata walimu wa dini waliokuwa wakifungisha ndoa hiyo na kuwachukua na kwenda nao hadi ilipo harusi na kuwakamata wengine huku wakiwapiga na kuwatuhumu kuwa wamehusika na ujambazi.
Hata hivyo polisi ilimwachia huru bibi harusi na kuondoka na babu harusi na wapambe wake sehemu kusiko julikana.
Miongoni mwa watu waliokamatwa ni Abdullah Saudi, Juma selemani, Saidi Ally na kassimu Othuman wote wakiwa wakazi wa Mbagala waliokuja kusheherekea harusi ya rafiki yao.
Chanzo: Jamii Forums
Polisi Yavamia Harusi, Wakamata Bwana Harusi na Watu Wake Kwa Kuhusishwa na Kesi ya Ujambazi Access Bank
2
February 29, 2016
Tags
Mwandishi sio uzuri kuandika habari kama vile unahisia waliokamatwa wameonewa na kuleta taharuki ktk jamii kama vile waliouliwa ktk ujambazi sio binaadamu fikiri kile kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na polisi hawataingia msikitini au kanisani na kukamata watu hovyo isipokuwa wana uhakika wanachokifanya jamani tuwe na ubinadamu sheria haichagui mtu awe padri au imamu achilia mbali waumini wasitumie udini kuficha uhalisi wao majizi au majambazi lazima washughulikie
ReplyDelete@anonymous 12:42 polisi washafanya uvamizi wa misikiti bila ya uhakika mara nyingi tu,polisi awafanya kazi yao kimaadili hilo lipo wazi tuu isipokuwa kuhusu suala hili yawazekana a walipata taarifa maana hao walichofanya ni kitengo cha kinyama na wanastahili adhabu kali cha muhimu wahakikishe wanakamata wahusika wa tukio na sio raia wema
ReplyDelete