Profesa Muhongo: Sijawahi Kupokea Rushwa wala 10% Ya Mwekezaji

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema hajawahi kupokea rushwa kwa mtu yeyote wala asilimia 10 ya wawekezaji wa miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Aidha, ametaka kuachwa kuingizwa kwa masuala ya siasa kwenye umeme, kwani umeme ni suala linalohitaji utaalamu zaidi na si maneno.

Alitoa kauli hizo juzi wakati akizungumza na wazalishaji wa umeme kwenye mkutano uliofanyika Mtera.

“Mimi hakuna mtu yeyote dunia nzima aliyewahi kunipa rushwa, nia yangu ni kuhakikisha taifa linapata umeme ikiwa ni pamoja na kuongeza wawekezaji, sihitaji hela ya mtu,” alisema Profesa Muhongo.

Pia alisema baadhi ya mitandao ya kijamii, imekuwa ikiripoti kuwa amewaita wazalishaji hao ili wamlipe asilimia 10 ; na kusema jambo hilo si la kweli hata kidogo.

“Kwenye masuala mengine ya mtandao ambayo hayana ukweli wowote muwe mnajitetea,” alisema Profesa Muhongo. “Acheni kuingiza masuala ya siasa kwenye umeme,” alionya.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndio maana Magufuli kakupenda na kukuweka hapo ulipo.
    HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  2. mh; tunategemea sana watanzania waishio vijijini watapata umeme na gharama za umeme kupunguzwa ili kuwawezesha wengi kupata nishati hyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad