Rais John Pombe Magufuli Atoa ya Moyoni Kuhusu Askari Watatu Waliofariki Jana Katika Ajali ya Gari


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Ernest Mangu kufuatia vifo vya askari watatu waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea jana tarehe 06 Februari, 2016 katika kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.


Askari waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Inspekta Miraji Mwegelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerald Ntondo.


Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na vifo vya askari hao, ambao wamekutwa na mauti wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.


"Kupitia kwako Mkuu wa Jeshi la Polisi natoa pole nyingi kwa familia za Askari waliopoteza maisha, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na askari wote wa Jeshi la Polisi Tanzania ambao wameguswa kwa namna ya pekee na msiba huu" Amesema Rais Magufuli.


Ameongeza kuwa anaungana na wote walioguswa na vifo hivyo katika kipindi hiki kigumu, na amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.


Rais Magufuli pia amewatumia salamu za pole Askari walioumia katika ajali hiyo, akiwemo Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani katika Mkoa wa Singida Mrakibu wa Polisi Peter Magira na kuwaombea wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

07 Februari, 2016

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ungepanda ndege wasingekufa
    Unatakiwa ushitakiwe kusababisha second mauder

    ReplyDelete
  2. Wewe ndo muajikwanini usipande helkopta

    ReplyDelete
  3. Mungu akulani Leo sina baba sina msaada wowote toka serikali ya CCM

    ReplyDelete
  4. Ulifikiri unabana matumizi Leo una cost maisha ya watu

    ReplyDelete
  5. Majibu ya wasiopiga mswaki
    ni ya kukurupuka tu kama nyie hapo juu.Hivi ni nani awezae kuzuia kifo?na ni wangapi walikuwa kwenye msafara mbona wasife wote?kutoka airport mkuu hahitaji escort?na jee ajali isingeweza kutokea?Any.7.18,Any.7.19 ni mmoja,POLE ila huna sababu ya kumlaani mtu yoyote kwenye hili.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuma wewe apande helkopta toka ikulu
      Anataka sifa sifa tu huyu
      Mtakufa wengi kumlinda ana nini rais Watanzania kiasi alindwe hivi
      Usalama WA taifa mmeoza Kabisa
      Hata mke WA waziri mkuu naye analinzi
      Hivi mume WA samia naye analinzi

      Delete
    2. Anonymous 12.40.
      Wewe umepitia wapi kuja duniani?
      Umemtukana mamako,dadako,shangazi yako.
      Hufai kuitwa binadamu wala kuishi,na kesho hutamka ukiwa salama usipotubu na kuona umekosea,utaamka umepooza mkono wako wa kushoto.nwasusikla gwalito nkooo ngahiko tiwsenabi bwee.

      Delete
    3. YAANI HUYU WA KUTUKANA MWANAMKE ALAANIWE KABISA.
      ROHO YAKE IACHE MWILI,HAFAI.

      Delete
  6. Alaaniwe kwa kumtukana mamake Na dadiye eti umekunywa maji gn filauni wee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad