Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.
“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.
Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.
“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.
“Kipindi kimoja kurusha ‘live’ kwa wiki mbili inatumika zaidi ya Sh bilioni nne, ni vizuri kuzikata hizo fedha zinazopelekwa kurusha ‘live’ zikapelekwa katika kesi za ubunge zinazohitaji shilingi bilioni tatu kusikilizwa hadi kumalizika kwake,” alisema.
Alisema mahakama ilikuwa inapewa bajeti ya Sh bilioni 41, lakini mwaka 2015/2016 ilishuka wakatakiwa kupewa Sh bilioni 12 ambazo hadi sasa hawajapewa.
“Kiongozi lazima ufikirie wapi pa kupeleka fedha na wapi pa kunyima, watu wa mahakama mnafanya kazi ya Mungu, nawaahidi ndani ya siku tano nitakuwa nimewapa Sh bilioni 12 zote.
“Sina tatizo la masilahi ya wafanyakazi wa mahakama, katika bajeti ya mwaka huu nitawapa fedha nyingi kuliko bajeti zote zilizopita, fedha zipo,” alisema.
Mahakimu Kutumbuliwa
Rais Magufuli alisema anamwagiza Jaji Mkuu kuwachukulia hatua mahakimu 502 ambao hawakufikia malengo ya kumaliza kesi 250-260 kwa mwaka. Walimaliza kesi chini ya 100.
“Mahakimu ambao hawajafikia kumaliza kesi 260 hayo ndiyo majipu yako Jaji Mkuu, unatakiwa kuyatumbua, wewe uliniapisha hata mimi, leo unapitisha agizo mwingine anapinga.
“Unatoa siku saba sasa sijui ndiyo watamaliza kutoa hizo hukumu, nakuagiza wachukulie hatua, tusipochukua hatua hakuna kitakachofanyika.
“Walioshindwa kufikia lengo unawabakiza wa nini, wasomi wako wengi, hata ukitangaza leo watajitokeza, niruhusu mimi nitangaze, sitaki kuingilia mahakama,” alisema.
Mabilioni ya NIDA
Akizungumzia hatua yake kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), alisema ilipewa Sh bilioni 176.6, lakini vitambulisho vilivyotengenezwa havifiki hata milioni mbili na havina sahihi wakati vitambulisho vya kupigia kura fedha iliyotolewa haizidi Sh bilioni 70, lakini vina sahihi za wapigakura wote wa Tanzania ambao ni milioni 23,253,982.
“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina, wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana, wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.
“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara kwa mwezi Sh milioni 35, naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.
Kesi za Wakwepa kodi
Rais Magufuli alisema kuna kesi 442 za kukwepa kodi ambazo zingeamuliwa Serikali ingepata Sh trilioni moja, ambayo ingeweza kununua ndege zaidi ya sita.
Alimuomba Jaji Mkuu kuzimaliza kesi 442 na kama zikimalizika fedha hizo Sh trilioni moja ataipa Idara ya Mahakama Sh bilioni 259 na Sh bilioni 750 zilizobakia zitanunuliwa ndege sita na wafanyafakazi 250 ATCL waliopo sasa wataondolewa.
Akizungumzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kuna kesi 26 za watu waliokutwa na nyara za Serikali, ambazo zipo zaidi ya miaka mitano hazijaamuliwa kwa sababu upelelezi bado.
“Polisi wapo, DPP yupo, upelelezi unaendelea kila siku, hapo unaona tatizo lilipo, DPP upo unapeleleza nini au unatafuta rushwa?” alisema.
Alisema suala la kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi ya wahujumu uchumi halihitaji kwenda bungeni kufanya mabadiliko, lifanywe haraka, mahakama ianze kwani nchi inachezewa.
Pamoja na hali hiyo Rais Magufuli alikubali kupokea maombi yote yaliyotolewa na mahakama na kuyazingatia kwani lazima ayaunge mkono ikiwamo kukubali watumishi wa Idara ya Mahakama wasome na kupatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
“Nimeamua nchi iende na itaenda, anayefikiria ataikwamisha atakwama yeye, nategemea zaidi mahakama katika kufanikisha hilo,” alisema.
Nilikuwa naichukia CCM kama donda ndugu haki ya Mungu,
ReplyDeletempaka rangi ya njano na kijani ilikuwa sumu kwangu,lakini naomba nikiri kwa mwendo wa Magufuli,kura yangu 2020 ni kwako Muheshimiwa(CCM) kama tu utagombea tena.Maana nikiangalia kwa wengine(UKAWA)sijui labda wamsimamishe mwingine lakini kama ni timu iliyopita nasema NO.kwenye hilo kundi la viongozi wao kuna mmoja kashika shamba kubwa kwa miaka mingi na wala haliendelezi limekutwa na msitu lakini kathubutu kuwanyang'anya wananchi waliojihifadhi baada ya mafuriko kwa kigezo eti analilipia,ana haki zote za kumiliki hata kama hakuna anachofanya kwa wakati huu,hapo ndipo nikasema kumbe wote ni hao hao tu,swala hapo ni kuchagua mtu sio chama.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI RAIS WETU,WEKA MKONO WAKO KWA WENZETU ZANZIBAR,AMANI IKATAWALE.
dah,umenitoa chozi mdau.Mungu akubariki na wewe pia.
DeleteAMEN!
DeleteTutakuelewa tu baba,tuvumilie usije ukafanya hasira ukajiuzulu kwa maneno ya wakaa kivulini ili wakukatishe tamaa waendelee kukaa kwenye neema sisi wa chini tukiteseka.
ReplyDeleteWatanzania ni kama tumerogwa,tumeshasau kama tulikuwa tunamuomba Mungu atupe kiongozi kama wewe,leo hii tunakutupia lawama kibao.Mungu akubariki.
Saaafi mzee wa wanyonge wewe ndio wa kuwafikiria sio hao kutwa kuwaza kwenda ulaya
ReplyDeleteUsipoheshimu mamlaka iliyopo kwa nini na wewe uheshimiwe,hapa kazi hufai pisha wengine wapo watanzania tumesoma wengi Tu, demokrasia bila udikteta kidogo hatuendi, Nchi itakaa sawa Tu ,Mungu akuongezee maarifa Mr JPM
ReplyDeletehakuna cha magufunyo wala bb yke magufunyo, yaliyo mengi yanawafkia wachache, mahakama zilzochache znatenda haki. n vzr huyu dogo akatulia tu maana utendaj wake hko dar es salaam tu ss vjjn shda tupu. Sasa atanidang'anya kwa lp?
ReplyDeleteAna muda gani?
DeleteYeye atajuaje kama wewe ulie kijijini hutoi taarifa kama kuna kero?
na WW Ni mmoja wao utanyooka Tu,rais akisema BC ujue hiyo Ni amri halali,we jizungushe usithubutu kukutwa ndio utaelewa anachomaanisha
DeleteRais Magufuli uje kenya kidogo.
ReplyDeleteJJP Magufuli, ongoza nchi baba atakaekuponda achana nae, tunaokupenda tupo.
ReplyDelete