Rais Magufuli Amteua Dr. Asha Rose Migiro Na Mathias Chikawe Kuwa Mabalozi Wapya....Dr. Kipilimba Kateuliwa Kuwa Bosi Mpya Wa NIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.

Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:

Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.

Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia.

Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni.

Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni orodha ileile ya Kikwete. Mugiro ni mtu simpati. Yupo kimya as if hana hewa. ninashangaa .

    ReplyDelete
    Replies
    1. UNATAKAJE?NILIDHANI UTASEMA ANA KASHFA FULANI.FYUUUUUUUUUUUU

      Delete
  2. Migiro aliyefukuzwa UN hajui kazi huyu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Una uhakika na unayoyasema?
      Alifukuzwa kwa lipi?tujuze.

      Delete
    2. Hajui kazi
      Kinabebwa bebwa tu don't have confidence bora mpeleke Kenya kungine hawezi
      Na pamoja Na ndugu radhia balozi Africa kusini

      Delete
  3. Balozi aliyefanya Na kuitangaza Tanzania UK na USA ni Mwanaidi
    Kwanini asirudi

    ReplyDelete
  4. Dunia nzima hakuna anamjuwa pamoja Na kufanya kazi 5 years
    Only Tanzania wanamjuwa
    Huyu anafaa Kuwa balozi

    ReplyDelete
  5. Tangu dada yake mwatumu malale, mdogo wako Radhia balozi Africa kusini hata wanabebwa tu , Na hata tulia alikuwa mwanafunzi wake wanaingia uozo mtupu serikalini
    Ulizeni dunia nzima Nani anajuwa migiro

    ReplyDelete
  6. Unyenyekevu wa kikondoo. Yes sir no sir.
    To be used by who ever above her. Atatimiza tu. Hii si sifa ya uongozi.Kiongozi safi awe huru, mwenye msimamo binafsi.
    Mgiro ni mtii wa amri tu. Kuna viongozi toka ukawa wazuri tu. Tatizo kuwaweka viongozi mizigo linaleta marumbanokisiasa na kiutendaji kazi. inarudisha pia maendeleo nyuma.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad