Rais Magufuli Apigilia Msumari Sakata la Zanzibar..Adai Hakuna Jinsi zaidi ya Kurudia Uchaguzi


Rais John Magufuli amesema kuwa hana mamlaka yoyote ya kuingilia suala la uchaguzi wa Zanzibar.
 

Rais Magufuli aliyaeleza hayo  jana katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga  jana ikulu jijini Dar es salaam.

 

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli aliwaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Alisema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

 

Alosema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

 

Alisema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

 

Aliwaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.

 

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio”ilisema sehemu ya hotuba hiyo.

 

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama huna madaraka ya kutatua huu mzozo bora ufunge bakuli lako, maana hata ushauri ni uozo. Kwa vile tu mmezoea kukanyaga katiba. Soma vizuri katiba inasemaje. Halafu mtu mwenyewe ulishindwa katika uchaguzi. Please, shut the fuck up!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani rais angemshauri bi kizee wako kule kwenu kijijini aache ushirikina kwani mafanikio yako yanafahamika kwa kutumia mandondocha ya ndugu zenu.Watu wabaya sana nyie.
      Mmuache mh.rais atekeleze majukumu ya kutumbua majipu na bado lile lakwenu kule Richard monduli!

      Delete
    2. Koma wewe Kwani Magufuli mungu
      Ni Mtu Kama Mimi Na wewe
      Urais ni dhamana tu
      CCM mu wapumbavu sana eti rais hahojiwi
      Nawasikitia sana walioipa kura CCM
      Magufuli he is ok lakini kwa CCM ni Kama nguvu ya soda

      Delete
  2. Hoja ya kurejewa uchaguzi ipo madhubuti JPM mtukaneni lkn kawambia ukweli hoja yenu ya Katiba dhaifu thibitisheni kama mlishinda ktk uchaguzi wa marejeo mnaopa nini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad