Rais Magufuli Uso Kwa Uso na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Waongelea Suala la Zanzibar

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi hapa nchini Mheshimiwa Jaji Damian Lubuva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa tume hiyo ipo huru na haijawahi kuingiliwa kimaamuzi na Rais wala kiongozi yoyote.

Jaji Lubuva amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli ambapo alikuwa akimpa taarifa juu ya yaliyojiri katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Mjini Kampala, Uganda na kujadili kuhusu uchaguzi Mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.

Amesema katika kikao hicho ambacho yeye alikuwa mwenyekiti, wamezungumzia umuhimu wa tume ya uchaguzi kuwa huru huku wakichukulia mfano wa Tanzania ambayo imetoka katika uchaguzi mkuu miezi michache iliyopita.

Jaji Lubuva amefafanua kuwa tume ya uchaguzi inapaswa kuwa huru katika maamuzi yake na kwamba jambo hili limekuwa likifanyika wakati wote hapa nchini.

Amebainisha kuwa wanaosema Rais anapaswa kuingilia kati masuala ya uchaguzi iwe Tanzania bara ama Zanzibar wanafanya makosa, kwani kwa namna yoyote Rais hana mamlaka hayo na hivyo hawezi kuingilia maamuzi ya tume hizo

“Unaposikia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano aingilie hilo suala la uchaguzi wa Zanzibar, yeye kwa kweli hana mamlaka kabisa. Pili ni kama kujikanganya, huku unasema tuwe na tume huru isiyoingiliwa halafu huku unasema aingilie kati maamuzi ya tume” alisema Jaji Lubuva

Jaji Lubuva amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikatiba hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar na hata huku bara pia hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume.

Mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi amewasihi Watanzania kuwa uchaguzi umekwisha, na kuwaomba waungane na viongozi waliochaguliwa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
01 Februari, 2016
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAWA ILA INAPOTOKEA VURUGU,UVUNJIFU WA AMANI KUTOKANA NA MAAMUZI YA KIDIKTETA YA TUME,WANANCHI WANAPOINGIWA NA HOFU KUU NA SHUGHULI NYINGI KAMA SIO ZOTE ZINASIMAMA,HAPO NDIPO MHESHIMIWA RAIS ANAINGILIA KUHAKIKISHA AMANI INAREJESHWA.JEE ANAHOJI CHANZO?ANAHOJI KILICHOTOKEA?ANATAFUTA MKOSAJI?[KUMBUKA HAPA MKOSAJI NI KIONGOZI-MMOJA TUU-WA TUME].ANAJIBIWA NA WANANCHI,ANAPATA UKWELI KWAMBA CHANZO NI UDIKTETA WA MTU-TUME.ANAFANYA NINI HAPO MHESHIMIWA RAIS? ANAKEMEA?ANACHUKUA HATUA? TUME HURU,HURU MAANA YAKE NINI?HAWA HAWAKUTOKA NCHI NYINGINE HAPANA NI RAIA WA NCHI WALIOTEULIWA[INAWEZEKANA KABISA KWA UPENDELEO NA AU LENGO MAALUM]WANA UTASHI WAO WA KISIASA,WANAMHESHIMU NA KUMUENZI BOSI ALIYEWAPA ULAJI HUO.JEE INAWEZEKANA UKAWAITA RAIA WATEULE NA RAIS KUWA TUME HURU?KWA UHURU UPI? TUSIJIDANGANYE,KWA LEO HII DUNIA INAIANGALIA CCM,DUNIA INAIANGALIA TANZANIA.KUWA WAKWELI PEKEE KUTATUPA UHURU KAMILI,KUWA WAKWELI PEKEE TUTAKUA KARIBU NA MOLA MUUMBA WETU,KUWA WAKWELI KUTATUPATIA HESHIMA KUBWA DUNIANI NA MBINGUNI KWA SABABU MKWELI DAIMA HUJIEPUSHA NA DHAMBI NA MWENYEZI MUNGU SIKU ZOTE ANAMJAALIA KWA NEEMA TELE-TELE MKWELI.

    ReplyDelete
  2. napenda nikuulize swali mheshimiwa jaji lubuva.hivi hapo ulipo kama mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi uliwekwa na nani?jee ulichaguliwa kwa kura za wananchi au uliteuliwa na mheshimiwa rais?nani ana uwezo wa kuutengua eteuzi huu,bunge?wananchi?au mheshimiwa rais? jee mheshimiwa rais magufuli akitaka kukufukuza kazi[kukutumbua jipu] kesho atahitaji kibali cha mtu mwingine?jee unajiita wewe kuwa unaongoza tume iliyo huru?masuali ninayokuuliza pia ni hayo hayo kwa zec-zanzibar kwa mwenzi wako jecha.mzee lubuva taaluma ya sheria ni taaluma inayohitaji ujasiri wa kutenda haki kwa kutanguliza ukweli,jitambue.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad