Kauli hiyo alianza kuitoa katika mahojiano aliyofanyiwa katika Kipindi cha E-News kinachorushwa na EATV ambapo alisema kwamba huwa anakwenda saluni mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) pia na kunywa maji mengi.
“Zamani ilikuwa shida kuingia saluni kufanya scrub, sasa hivi najiweza katika hivyo vitu, kwa hiyo kwa kila wiki lazima nifanye scrub, nijitengeneze mwili wangu kama kioo cha jamii ninapotokea katika TV ili wewe Mtanzania uweze kuni-admire, kwa hiyo kimsingi sijichubui, nafanya sana mazoezi na kunywa maji mengi ndiyo siri ya ngozi yangu kunawiri,” alisema Ray.Jamii kwa ujumla ilimchukulia tofauti na gumzo lililoenea kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na mashabiki wake wengi kufanya jaribio la kunywa maji mengi kwa mara moja huku wengine wakiunda makundi na kujiita Team Water Baby (TWB).
Showbiz Xtra ilifanikiwa kufanya mahojiano na Ray ambapo katika makala haya anafunguka yote;
Xtra: Kauli yako ya kufanya mazoezi na kunywa maji mengi, watu wengi wameichukulia tofauti, unazungumziaje hilo?
Ray: Siwezi kuwaongelea sana kwa sababu kila Mtanzania ana haki ya kuzungumza kile anachokiwaza kichwani kwake, kikubwa ninachoamini maji ndiyo yananifanya niwe na ngozi nyororo, basi! Kwa hiyo nafanya sana mazoezi na nikwambie tu hilo la kunywa maji mengi kama hawawezi basi siwezi kuwakataza ama kuwalazimisha kwangu inawezekana ndiyo maana naendelea kuwa mweupe. Hata kwenye familia yetu hakuna mtu mweusi na kama atatokea mweusi atabakia kuwa mweusi na kama mweupe atabakia kuwa mweupe.
Upuuzi mtupu kwani ukiwa mweupe ndo haufi?au utaenda peponi?africa bado sana wacha wazungu waendelee kutucheka.
ReplyDeleteHakuna cha maji wala upuuzi wa maji, huyu mtoto anakula mkorogo kama kawaida ya wanaojichubua. Kama ni maji basi anayatumia kunywea vidonge vya kujichubua kama wazaire wanavyosema.. Asituletee ujinga wake wa kutaka kuwa mweupe kama mzungu.. apeleke ujinga wake huko kwa wabongo movi wenzie
ReplyDeleteDaRay bado maboobs na makalio saiv hujatia mana tayar mweupe ushanyowa nyusi na ushatia nywele kali.
ReplyDeleteIli wachumba waje walete posa kwenu.
ReplyDeletekubwa zima hovyo we ngozi yako tunaijua ni nyeusi we ulikuwa kama baracka da prince
ReplyDeleteleo uko kama marehem michael jackson
ebu kasome vizuri faida za maji kwa ngozi
tatizo elimu sijui me bongo movie imeishia kula mkorogo
mkoroooooooooooooooooooooooooooooooogo. demu wake ana moyo maana wanashare vipodozi.
ReplyDeleteOk ungenyamaza bora au kufikiria movie nyengine hizo nyusi na wanja
ReplyDeletekama hamtaki si basi ... na nyinyi jaribuni kujua ukweli
ReplyDelete