Serikali ya Magufuli Inajiandalia Anguko Kama Sio Aibu Siku zijazo

Dhana ya utumbua majibu inayoonekana kufanywa kwa nia njema na wakati mwingine kwa dhamira ya kisiasa zaidi bila kuchukua kwanza tahadhari ya kutosha,inaiweza kuja kuiweka serikali hii katika mtihani mgumu sana siku za usoni pale mambo yatakapoanza kuharibika na watu kuanza kukimbiana na wengine kugeukana.

Ziko sababu kadhaa zinazoweza kuja muifanya serikali iiumbuke ikiwa ni pamoja na kushindwa kesi pale itaposhitakiwa.

Makosa ya serikali yenyewe
Kuna baadhi ya shughuli za serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma zimefanywa chini ya kiwango au kutotekelezwa kabisa kutokana na serikali kupeleka fedha kidogo tena kwa mafungu mafungu na wakati mwingine kutopelekwa kabisa licha ya kuwa Taasisi husika ilitengewa bajeti. Hili linaweza kuja kujitokeza katika Taasisi kama Bodi ya Mikopo na nyinginezo ingawa ursasimu,uzembe na utendaji mbovu wa watumishi unaweza kuwa sehemu ya tatizo

Influence ya wanasiasa
Kuna sehemu watendaji wanawajibishwa lakini mwisho wa siku uchunguzi unaweza kuja kubainisha kuwa kulegalega au utendaji mbovu katika Mashirika / Taasisi hizi kumechangiwa na maamuzi ya wanasiasa kuingilia utendaji wa ma-CEO,manegement na hata Bodi zinazosimamia Mashirika haya na hivyo itafika wakati baadhi ya ma-CEO hawa watakuja kuonekana hawana hatia na kulazimika kurudishwa kazini au kupangiwa kazi nyingine.

Sheria za Utumishi wa Umma
Kuna watendaji leo hii wanaweza kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi lakini taratibu na sheria za utumishi zikifuatwa,huenda baadhi yao ikaja kuonekana kuwa waliadhibiwa kimakosa na Mahakama ya kazi inaweza kuagiza warudishwe kazini mara moja.Serikali inabidi na ilipaswa kutazama vizuri sheria hizi za utumishi wa umma na kuzirekebisha kwanza kabla ya kuendelea na fukuzafukuza hii au huku kusimamisha watu kazi kila kukicha.

Agenda za Kisiasa
Wakati unakuja siasa hazitakwepeka katika hili zoezi la utumbuaji majipu. Wanaotumbuliwa waliwekwa na wanasiasa na wanaowatumbua ni wana siasa ila nao wana ya kwao hivyo itafika hatu mmoja akimwaga ugali mwingine atamwaga mbogo kwani sidhani kama kuna msafi miongoni mwao na wataanza kutoleana siri.

Wanaotumbuliwa kuamua kutoa ya mayoni:
Kuna baadhi ya wanaotumbuliwa ambao mambo yao yanaweza kuja kuisha kiani iwapo wataamua kufunguka kiasi cha kutaja majina makubwa na pale itakapoonekana mambo yameisha kiujanjaujanja, ndio serikali itajikuta ikiinyooshewa kidole na pengine hata kusutwa.Hawa wanaotumbuliwa wanaweza hata kupenyeza siri kwa waandishi wa habari.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
Kushinda kesi nyingi zitakazoibuka hapo baadae kufuatia maamuzi yanayofanywa sasa na serikali,itategemea na ufanisi na uwezo wa Ofisi hii kusimamia kesi ambazo serikali inaweza kushitakiwa.Kama watakuwa hawajajipanga vizuri kwa kuwa na wanasheria competent na wa kutosha huku serikali ikikabiliwa na kesi nyingi,kuna hatari ya serikali kuja kushindwa kesi nyingi zitakazifunguliwa na watumishi,watu binafsi ama makampuni.Katika kipindi hiki, Ofisi hii inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko Taasisi nyingine yote ya umma.

Ukifukuza watumishi,ukinyang'anya watu mashamba,ukivunjia watu nyumba na ukanyang'anya watu leseni,ofisi pekee itakayobeba mzigo wa kesi zitakazofunguliwa ni hii ofisi ya AG labda kama kuna utaratibu wa serikali kuweza kukodi makampuni binafsi ya uwakili kuisadia kusimamia baadhi ya kesi zitakazofunguliwa.

Maamuzi ya bila umakini
Hivi sasa mawaziri wako busy kusimamisha watu kazi na sidhani kama wanachukua tahadhari ya kutosha kabla ya kufikia maamuzi haya.Mfano mzuri ni kusimamishwa yule mtumishi aliyekuwa kiongozi wa bomoaboma alafa baada ya siku chache ikitako taarifa kuwa amerejeshwa katika nafasi yake(kama sikosei Nipashe ndio iliripoti habari ya mtumishi huyu kurudishwa kazini).

Kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya serikali ni jambo jema na linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo, lakini katika zama hizi za haki za binadamu na utwala wa sheria plus sheria zetu za utumishi wa umma, maamuzi haya ya leo yanaweza kuja kuwa "counterproductive " kwa serikali yenyewe yasipofanywa kwa umakini na kwa kutaka kujijenga kisiasa.

Katika kesi/mashauri kumi,serikali inatakiwa kushinda si chini ya saba au nane tofauti na hapo itakuja kuishi kubezwa kuwa ilikurupuka.

By Salary Slip/JF

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe acha Magufuli afanye kazi yake, ulitaka afanye nn? awaachieni mkifanya upuuzi wa kutafuna mali za umma? kuna vitu vingine vinakera mpaka mheshimiwa anakuwa anafanya maamuzi hayo, kuna watu wanafanya vitu vyakijinga kabisa kama vile siyo wasomi, wanaudhi kwakweli hata wakitumbuliwa ni sawa tu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dole wandio wasema kweli waache kutubabaisha ya ugali ya mboga yanawahusu wao tumechoka na dhuluma wamwache Magufuli afanye aliyotumwa na kuwaahidi watanzania wengine kelele za mlango

      Delete
  2. Hivi wewe n mtz kweli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. ningekwepo nae karibu ningemtwanga makofi huyuu mwanshii choo kweli anatetea ujinga

      Delete
  3. Ikianguka tutaanguka nayo ikiingia tutainuka nayo acheni woga na msimix Mambo.Rais na serikali yako piga kazi

    ReplyDelete
  4. Wewe mwandishi una rahana kam una rahana karahaniwe.

    ReplyDelete
  5. Nyie mnaoshadadia yatawakuta soon magu hachagui mnyonge wala fisadi nyie subirini mi yangu macho akishaliza mafisadi atarudi kwa wanyonge maana yeye anataka sifa 😂😂😂mwaka huu wataisoma...2020 hapiti ng'ooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na JPJM ameshasema kuwa kama mtu unajiona una jibu,jisalimishe,lakini watu mko kimya.
      Unaamini anataka sifa na sio kusaidia wananchi?Sawa sio mbaya kwetu sisi wananchi walala hoi,tunaomba na tunamuombea aendelee hivyohivyo.Mungu Mbariki rais wetu na mawaziri wote.

      Delete
  6. umesahau pia huyo mbaba hakuhudhuria mikutano muhimu mwanzoni mwa uwajibikaji wake na malofa wengi tu wakasema haina shida!

    ReplyDelete
  7. Hakianguki kitu hapa.Mheshimiwa kaza kamba mungu yu nawe. Hakuna atakayekutwa kama utakula jasho lako na kuwa na uadilifu kazini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. 5 mdau.Magufuli anainua serikali iliyoanguka kwa miaka kadhaa sasa,na ni kweli kama mtu anatafuta pesa kwa njia halali hatakumbwa na haya majipu.Tumuombee sana huyu
      rais wetu.

      Delete
    2. Na sijui kwa nini hakugombea zamani,pengine tusingefika hapa tulipofika.Any way wanasema kila jambo lina wakati wake.MUNGU MBARIKI MAGUFULI

      Delete
  8. Asipopita utapita wewe lkn kazi ifanyike tu

    ReplyDelete
  9. Mungu tunakuomba msimamie rais Magufuli.
    iko mijitu kila wakiguswa majipu kama si ndugu zao asubuhi wanaandika magazetini kumkatisha tamaa rais wetu.
    Si mjisalimishe wenyewe,mkubali kutaifishwa mali zenu muone kama.MCHUMIA JUANI HULIA KIVULINI NA MCHUMIA KIVULINI HULIA JUANI,kwa nini hamuogopi mali za longolongo wakati hata Mungu katuambia kwa jasho letu tutakula?VIVA MAGUFULI.

    ReplyDelete
  10. Mmmmh! Ushindwe kwa jina la yesu wewe unayetaka kuzima kasi ya Magufuli.

    ReplyDelete
  11. Kuna mtanzania maskini asiyemuombea kwa Mungu huyu rais wa awamu ya tano?Anza sasa hivi maana ana vita kubwa sana kutoka kwa machori,ni Mungu tu ndio anamuepusha na mabalaa.
    JPJM tunakuombea sana na vita utashinda.

    ReplyDelete
  12. Salary slip/JF una lako jambo.

    ReplyDelete
  13. DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE.
    HAKIANGUKI KITU HAPA.
    TENA MIMI NATAMANI AKITOKA MAGUFULI WANAJESHI WATUSHIKIE AWAMU YA SITA,WATUNYOSHE VIZURI,TULIJISAHAU MNO.KHAAH!

    ReplyDelete
  14. BAADHI YA WATANZANIA NI WATU WA AJABU SANA YOTE HAYO WIVU TU MBWA HAWA ASINGECHUKUA HATUA HIZI PIA ANGEONEKANA HAFAI HAWA MBWA TU

    ReplyDelete
  15. Magufuli Usikubali Kugeuka Nyuma,Mbele Kwa Mbele.... Safisha Takataka Zote....hata sisi walala hoi km hatufati Sheria, Safisha Tu !.... Wewe Ni Mzalendo Wa Kweli, Una Uchungu Na Watu Wa Nchi Hii....Mungu Akulinde Na Awashinde Maadui Wanaokutizama Kwa Jicho Baya!.....HIVI KUMBE TANZANIA BILA UNYANYASWAJI KWA WANYONGE, INAWEZEKANA ??? .....Mungu Umlinde Magufuli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad