Shahidi wa Paul Makonda Ajichanganya kortini Kesi ya Kubenea Kumtukana Makonda..

DENIS Mujumba, Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ambaye pia alikuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni amefura baada ya kuulizwa maswali wakati akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya jinai inayomuhusu Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Ltd na pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo. Anaandika Faki Sosi.

Mujumba (39) amefikwa na masaibu hayo baada ya kubanwa kwa maswali na Peter Kibatala ambaye ni wakili wa Kubenea wakati akitoa utetezi wake huku hakimu wa kesi hiyo kwenye Mahakama ya Mkazi Kisutu Thomas Simba akimtaka kupaniki.

Kesi hiyo ambayo Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndiye mlalamikaji, ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi hao wawili kugombana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana.

Wakili Kibatala alimuuliza Mujumba kama ni yeye ndiye aliyekutana na baadhi askari polisi kwenye eneo la tukio na je alikuwa anawafahamu na pia walikuwa chini ya nani? Mujumba alijibu kuwa, aliwakuta askari hao eneo la tukio na kumuongeza kwamba, hakujua walikuwa chini ya nani.

Kibatala: Wewe ndio mwenye wajibu wa kuchunguza kesi hiyo je wewe ndio Mkuu wa Mkuu wa Idara hiyo?

Pia aliuliza kwamba siku hiyo kulikuwepo na waandishi lakini alipataje picha za video na sauti kutoka kwa waandishi wa habari?

Mujumba: Ni kweli kulikuwepo na waandishi na kwamba niliwasiliana na waandishi hao ili wanipe ushahidi wa picha, sauti au video. Waandishi walinijibu kuwa hawana ushahidi huo.
Kibatala: je ulikwenda na askari wangapi?

Mujumba: nilikwenda na askari wanane au tisa.
Kibatala: wataje majina
Mujumba: Ni Sajenti Peter, PC Hamis, Joachim na Doel.
Kibatala: Shahidi hajui askari wake kwani anajua jina moja tu la mwanzo na hajataja wote.
Maswali haya yalisababisha Mjumba kukunja sura na kutoa sauti ya juu huku akitaka kubishana, Hakimu Simba alimwambia “acha kupaniki” na kumtaka aache kubishana na wakili.
Hakimu Simba pia alimwambia Mujumba kwamba hana uwezo wa kubishana na wakili huyo na kuwa, anachotakiwa ni kujieleza kwa kujiamini.

Wakili Kibatala kwa kutumia sheria Namba 155(a) aliiomba mahakama kuonesha picha za ushahidi zilizokuwa zianonesha hali halisi ya tukio.

Wakili huyo aliinesha mahakama picha ambazo zilionesha kuwepo kwa askari walioshika bunduki na kumzingira Kubena, kwenye picha hiyo Mujumba hakuwemo.

Hapo awali Mujumba aliieleza mahakama kwamba yeye ndiye aliyemsihi Kubenea aende naye kwenye Kituo cha Polisi Magomeni, hivyo Wakili Kibatala aliongeza kuwa, kwa kutokuwepo kwenye picha ile Mujumba alitoa maelezo ya uongo. Hakimu Mkazi hata hivyo, baada ya shahidi huyo kutoa ushahidi wake, Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo hadi tarehe 15 na 16 Aprili mwaka huu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad