Wanandoa mbalimbali wakishiriki kwenye michezo inayohamasiha upendo na mshikamano wakati wa maandalizi ya kusherekea siku ya wapendano ambayo iliambatana na uzinduzi rasmi wa chapa mpya za “Fiesta condoms” nchini Tanzania. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Washindi wa safari ya Cape town Bw & Bi. Mohammed wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa shirika la DKT International nchini Tanzania Bw. Raphael Da Silva (Kulia) mara baada ya kuibuka washindi kwenye bahati nasibu iliyochezeshwa wakati wa uzinduzi rasmi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa shirika la DKT International Tanzania Bw. Davis Kambi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza jijini Dar es salaam. Washindi hao walijishindia safari za mapumziko kuelekea Zanzibar, Cape town na Dubai.
PRESS RELEASE
Februari 2016, Dar es Salaam Tanzania
Shirika la kimataifa la DKT, linalojihusisha na elimu ya uzazi wa mpango pamoja na vita dhidi maambukizi ya VVU na UKIMWI, hivi leo limezindua kondomu za Fiesta katika soko la Tanzania.Kondomu za Fiesta zimekuwa sokoni kwa zaidi ya miaka 20 na zinapatikana nchi zaidi ya 40 duniani kote. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Ledger Plaza maeneo ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu umekuja kipindi kifupi kabla ya sikukuu ya wapendanao duniani ya Valentine ambayo pia ni siku ya kimataifa ya uelewa wa kondomu.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, meneja masoko wa DKT International nchini Tanzania, Bwana Davis Kambi alisema anaamini ni muda muafaka kwa chapa hii kupatikana katika soko la Tanzania.
“Huu ndo utambulisho rasmi wa chapa hii Tanzania ikiwa kama njia ya kukabiliana na mahitaji ya wateja wetu na kuvutia watumiaji wapya” alisema wakati wa uzinduzi. Pia alisema uzinduzi huo utawapa wapendanao chapa wanayoweza kuiamini na itakayoboresha maisha yao. Wakiwa wameweka mikakati ya kuipa nguvu chapa hii kwa kutumia njia za mawasiliano na ushiriki katika nyanja mbalimbali ili kumrahisishia mtumiaji kuielewa na kuikubali chapa hii kama kitu poa kutumia.
“Kondomu za Fiesta ni mahususi kwa wapendanao ambao husaka raha na hisia kali zaidi. Fiesta ni sherehe yenye nakshi, Fiesta ni kwa ajili ya ukaribu zaidi. Fiesta ni chapa ya kisasa inayoshindana na chapa nyingine za kondomu kubwa kimataifa” alisema Kambi.
Fiesta ina zaidi ya ladha 55 tofauti na zaidi ya aina 60 lakini kwa sasa DKT International Tanzania imetambulisha aina nne tu; Fiesta Heat, Fiesta Ultra-thin, Fiesta Strawberry and Fiesta Max dotted. Aliongezea kwa kusema kuwa shirika linatazamia kuongeza aina tatu (3) zaidi kabla ya kufikia mwisho wa mwaka 2016.
Kambi alisema uzinduzi huu wa kondomu za Fiesta utatengeneza historia kwa kuunga mkono juhudi za kufikia lengo la kuzuia maambukizi ya VVU kabisa. Alisema katika kulinganisha tafiti za VVU ya mwaka 2007-08 na Malaria 2011-12 nchini Tanzania, wamebaini kuwa maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 5.1 kati ya watu wenye miaka 15-49. Vivyo hivyo maambukizi yamepungua kwa wanawake kutoka asilimia 6.6 hadi 6.2 na kwa wanaume kutoka asilimia 4.6 hadi 3.8 na kama shirika linalopambana na VVU na UKIMWI katika dhana zote wanaendelea kuona haja ya kupunguza uenezaji wa gonjwa hili.
Aliwashauri watu wakumbuke kuwa kondomu husaidiaa kuzuia maambukizi ya VVU na hivyo ni muhimu kutumia. Aidha Kambi aliasa kuwa ni muhimu kondomu kupatikana kiurahisi na kwa bei poa ili kuvutia watumiaji wengi kitaifa.
Alielezea zaidi kwamba Fiesta zitapatikana kwa bei ya rejareja ya shilingi 1500 za Kitanzania ambayo ni kwa paketi ya kondomu tatu ambayo kiuhalisia ni bei rahisi kwa chapa ya kimataifa. Kwanzia mwezi huu zitapatikana maduka ya madawa, maduka makubwa ya rejareja, hoteli, gesti na klabu za usiku kubwa nchini kote. Alisema pia kwamba wanafanya kampeni maalum ya kuitambulisha zaidi Fiesta kwa soko la Tanzania.
Kwa maelezo zaidi:
Tovuti ya Trust: www.trustlife.co.tz
Facebook: http://www.facebook.com/Trustlifetz
Twitter: @trustlifetz
Instagram: trustlifetz