Soma Jinsi Tundu Lissu Alivyomlipua Magufuli Kwa Kusema Siku 100 za Ikulu Rais Amelikimbia Jukumu la Zanzibar

Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni mwanasheria wa (CHADEMA)Tundu Lissu amesema siku 100 ambazo Rais Dkt.John Magufuli kuwa madarakani amenyamaza kabisa kuhusu Zanzibar huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiwa vimeongezwa Zanzibar.

Lissu ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na EATV kuhusu tathmini yake kwa siku 100 ambazo Rais Magufuli amekaa madarakani ambapo amesema suala la ulinzi na usalama wa nchi hii linaongozwa na yeye hivyo kukaa kimya ni kukwepa jukumu lake.

''Yeye kama amiri jeshi mkuu hawezi kujitoa katika hili kwa sababu vyombo vyake ndivyo vimetoka bara kwenda huko kisiwani Zanzibar kuwanyamazisha wananchi hivyo hawezi jitoa katika suala hili kwa namna yeyote''Amesema Lissu.

Lissu ameongeza kuwa wakati vikao vya Bunge vikiendelea mjini Dodoma, Waziri Nape alitangaza kusitishwa kwa matangazo ya bunge kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na badala yake yatakuwa yanarekodiwa na kutafutiwa muda wa ziada, wakati matangazo hayo yamerushwa live kwa miaka 10

Aidha suala la kukamata makontena hatujawaona hao ambao wamakwepa kodi na hatua zilizochukuliwa wakati sheria za nchi zinasema kukwepa kodi ni kosa la jinai, pia suala la kutosafiri na kusema amekwepa gharama si kweli kwani wakuu wa mikoa,wakurugenzi na wakuu wa wilaya ni walewale na wakikwepa kutumia ndege mafuta wanayotumia kutoka Dar kwenda mikoani gharanma iko pale pale.

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu nae akili zake Ni tundu kama jina lake, hku nchi inasonga mbele WW bk na la Zanzibar, lilishatolewa ufafanuzi subiri uchaguzi WA marudio

    ReplyDelete
  2. Hayupo hiru. Hizi pilikapilika za huku na kule ni ndogo sana.bado amewakumbatia wakubwa ambao ndio chanzo cha taka zote nchini.anawaogopa na kuwakwepa. Ni hawa wanaojitokeza hadharani na kujidai watamsaidia na kumuunga mkono.wamijua hasa wao ndio majipu makuu nchini. Hayupo huru.asipoweza muwazatiti hawa na kuwa hukulia hatua kali hatafika mbali kiuongozi. Lete katbs ya nchi ndugu zmagufuli na utende haki kwa Watanzania na si kuwadanganya na kuashika dagaa tupu huku madingi wao unawasikiliza kama hujui kuwa ni majipu makubwa.onfoa kinga za maraisi wanaozidi kuipotosha nchii hii hasa kupitia.Zanzibar.hili ni jipu umelikwepa kama raisi kiongozi wa muungano. No mmuungano gani Mtoto wako moja umemwekea mtutu kumtishia na kujikosha huhusiki. Bado wanaiendesha Ikulu na nchi ukiwa kamakiongozi lakini ni mtoto wao wanamulisha makande. Analosema Lisu ni ukweli mtupu.hatujui agenda yako binafsi na msimamo wamo binafsi uko vipi.sheria za nchi pia bado hujawaburuta hao wanasheria waliokalia viti awamu ya nne wakiangalia nchi inachezewa kama choo. Hujawazatiti pia. Lazima hawa wawe mfano kwanza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. USIWE MPUMBAVU WA KUFIKIRI, TAJA HAO ANAOWAKUMBATIA MAANA NI WAKATI WA KUSEMA UKWELI NA UWAZI SIYO KUROPOKA VITU AMBAVYO HUNA UHAKIKA NAVYO. WALE WALIOFUKUZWA WOTE NI DAGAA?????? ZANZIBAR WATAMALIZANA NA HILO LILISHATOLEWA UFAFANUZI SASA KAMA AKIRI YAKO NI FINYU ENDELEA KUWA FINYU MPAKA CHINI YA UNYAYO WAKO

      Delete
  3. Replies
    1. U SURE WA LISSU UKO WAPI? AU HUJUI UNACHOKIANDIKA? RUDI DARASANI ILI UKAANZE UPYA KUFUNDISHWA. ZANZIBAR INA SERIKALI YAKE WAACHENI WATAMALIZANA

      Delete
  4. Lissu level ingine. namkubali sana! Rais pombe anakaa kimya kuhusu zanzibar bila kujali kuwa nchi inapoteza sura yake ya kuwa nchi ya demokrasia kwa mambo kama haya ya kufuta uchaguzi bila kujali kuwa ulikuwa wa haki na huru bali tu kwa sababu ccm ilishindwa vibaya.

    ReplyDelete
  5. Lissu level ingine. namkubali sana! Rais pombe anakaa kimya kuhusu zanzibar bila kujali kuwa nchi inapoteza sura yake ya kuwa nchi ya demokrasia kwa mambo kama haya ya kufuta uchaguzi bila kujali kuwa ulikuwa wa haki na huru bali tu kwa sababu ccm ilishindwa vibaya.

    ReplyDelete
  6. Rais si mungu
    Na hata mungu naye hukoselewa
    Kwani ukiwa masikini unasema mungu nimekukosea nini mbona wenzangu ni matajiri
    Sembuse kiji magufuli
    CCM Acheni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha uchizi mbwa we utamfananisha Mungu na Mwanadamu? pumbavu zako, kwanza mwacheni Rais wetu na inawezekana mna hasira naye kwa sababu si ajabu ndugu zenu wametumbuliwa majipu au wanangoja kutumbuliwa, msitafute kiki kupitia JPM

      Delete
  7. Tundu nae anatafuta kiki tuachen na magufuli wetu nyie simlisema hamumtambui

    ReplyDelete
  8. Huwezi kumfurahisha kila binadamu hata mungu wanamkosoa kisa mvua imenyesha mda wa saa5 sembuse rais,mwacheni apige kazi

    ReplyDelete
  9. wajinga ni media hivi kwa nini mnawatafuta wapinzani kutoa tathimini ya magu hamuoni kama wapinzani ni mataila??? hawana pointi juu ya jambo lolote hata bungeni kazi yao ni kuzomea zomea tu na kuleta vuvugu na siyo kuweka hoja tunajilaumu kuwachagua wahuni kutuwakilisha bungeni na kama tukirudia uchaguzi kesho wangebaki na viti vinne bungeni
    media mkitaka kujua tathmini ya utendaji wa magu njooni mitaani siyo kuwatafuta hao mataila ambao hata baraza lao la mawaziri ni utumbo wa neputisim

    ReplyDelete
  10. wajinga ni media hivi kwa nini mnawatafuta wapinzani kutoa tathimini ya magu hamuoni kama wapinzani ni mataila??? hawana pointi juu ya jambo lolote hata bungeni kazi yao ni kuzomea zomea tu na kuleta vuvugu na siyo kuweka hoja tunajilaumu kuwachagua wahuni kutuwakilisha bungeni na kama tukirudia uchaguzi kesho wangebaki na viti vinne bungeni
    media mkitaka kujua tathmini ya utendaji wa magu njooni mitaani siyo kuwatafuta hao mataila ambao hata baraza lao la mawaziri ni utumbo wa neputisim

    ReplyDelete
  11. acheni kuwa wavivu wa kufikiri. hv mumejibandika uzoro ndio muweze kushambulia wenzenu. Magufuli amefeli katika siku 100 na suala la zanzibar litammaliza. Kikwete amelitupa kwa magufuli baada ya yeye kushindwa,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad