Uchaguzi Mameya Kinondoni na Temeke sasa Kurudiwa

Uchaguzi wa umeya katika Manispaa za wilaya za Temeke na Kiondoni utarudiwa baada ya kugawanywa na kuzaa wilaya za Ubungo na Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, alisema Rais John Magufuli ameridhia kuanzishwa kwa wilaya hizo pamoja na mkoa mpya wa Songwe.

Aidha, alisema ameridhia kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Kibiti (Pwani), Malinyi (Morogoro) na Tanganyika (Katavi).
Alisema mchakato wa kuanzishwa kwa maeneo mapya ya utawala ulihitimishwa kwa kutolewa na tangazo la serikali kwa GN 69 ya Januari 29, mwaka huu, ya kuanzisha kwa mkoa wa Songwe na GN namba 68 ya kuanzishwa kwa wilaya za Songwe, Kibiti, Ubungo, Kigamboni, Malinyi na Tanganyika.

Simbachawene alisema Mkoa wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa sheria, hivyo hivyo kwa wilaya za Songwe, Kibiti, Ubungo, Kigamboni, Malinyi na Tanganyika.
Kuhusu uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, alisema utarudiwa Februari 8, mwaka huu.
Alisema baada ya kugawanywa kwa wilaya hizo ni dhairi kuwa, baadhi ya madiwani itabidi wakae kwenye halmashauri zao ambazo zinaanzishwa.

Alisema hivi karibuni atateua wakurugenzi wa halmashauri hizo na baadhi ya watendaji muhimu.
Simbachawene alisema amewaagiza wakuu wa mikoa wote ambao katika mikoa yao imeanzishwa wilaya mpya kufanya maandalizi muhimu ili kuwezesha mikoa na wilaya hizo kuanza rasmi.
Katika agizo hilo, ameweka mkazo uwekezwe kwenye upatikanaji wa majengo ya ofisi na huduma muhimu ili kuweka mazingira ya shughuli za kiutawala kuanza kufanyika katika maeneo hayo ya kiutawala.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad