Ukata Wamkumba Ray C, Adai Analazimika Avae ‘Ninja’ ili Aweze Kutumia Usafiri wa Daladala....Aomba Msaada Kwa Wenye Uwezo

Msanii wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema hali yake ya uchumi imekuwa mbaya zaidi hadi anashindwa kumudu baadhi ya gharama za maisha yake.

Muimbaji huyo ambaye yupo kwenye tiba ya methadone katika hospitali ya Mwananyamala kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television Jumatatu hii kuwa, anatamani sana kurudi kwenye muziki ili apate kipato chake lakini anashindwa.

“Jamani kiukweli haya maisha ya wasanii nyie acheni tu, yaani inabidi tumuombe tu mungu, mtu akikuona msanii kwenye daladala nani atanunua albamu yako, nani atakuja kwenye show yako, lakini mama ananiambia vaa ninja mwanangu nenda kapate tiba. Kwa sababu kila siku kukodi taxi ni gharama sana, kutoa elfu 25000 kutoka Bunju mpaka hospitali kila siku ni nyingi sana. Sometimes namwambia mama inabidi tutoke mapema saa 11 hivi nivae ninja twende kwanza kanisani then naweza nikachukua hata bajaji kwenda hospitali. Haya ni maisha sio kitu cha kucheka ni lazima nifanye hivyo ili niweze kumaliza dozi,” alisema Ray C.

Pia Ray C ameomba wadau mwenye uwezo wamsaidie kupush muziki wake ili aweze kujisaidia mwenyewe.

“Hakuna masharti yoyote kwenye kunisaidia, mpaka mtu akitaka kuchangia, sijui elfu 10000, 2000, jamani unaweza kunisaidia kwa namna yoyote, kiukweli mimi nahitaji kurudi kwenye game na mtu ambaye alitaka kunisaidia ameniacha,” alisema Ray C.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole ray c jamani daaah Mungu akusimamie maisha haya si yakumcheka yani yanabadilika ndani ya masaa...vipi NGO yako imeishia wapi dada ray c

    ReplyDelete
  2. Nakumbuka raisi mstahafu alikusaidia sana,mpaka mama yako akasema hauitaji tena msaada wa mtu yeyote!! Kwa kifupi mtu wa kukusaidia niwewe mwenyewe. Watanzania wengi mnachezea maisha yenu. ( Mimi ni mtanzania lakini sasa hivi ninaishi ughaibuni.)Sasa chagua moja, chagua maisha ua kifo, usilete usanihi katika maisha. JB USA.

    ReplyDelete
  3. Kwa mfano mtu ameisoma hii habari ya Rehema Chalamila ikam touch na anataka kutoa donation kwake lakini huyo mtu haishi Tanzania anaishi nje Je afanyeje ili hiyo danation imfikie huyo muhusika?maana kwenye hiyo habari contact zake hazikuwekwa so itakuwa ngumu kusaidiwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. +255768009715 mtafute kwa hi number via Watsapp or call me binafsi nimeguswa. Ubarikiwe

      Delete
  4. Kama kweli kaongelea hizo shida zake tupeni contact zake tumtumie pesa isije kuwa magazine

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtafute kwa hi number +255768 009715.

      Delete
  5. Lakini jamani mkumbuke kwamba hawa ni watu ambao hatakuolewa walikuwa nataka mikataba, mungu ananjia nyingi za kuuonye yeye ni mungu. Kwahiyo dada ushauri wangu ni kwamba unaweza pata kazi sehemu yoyote na ukapata mshahara mzuri, zamani ulikuwa unatangaza kwanini usiombe kazi ya utangazaji, try something else ya income doesn't have to be music labda mungu anataka upate ridhiki yako kwa njia nyingine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We we hakuna msafi duniani na Mungu anasamehe acha ushauri wa kikejeli unadhani rahisi kupata kazi wakati hajamaliza dozi. Wewe ni binaadamu Kama sisi yote mapito na mafunzo!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad