Utafiti: Umaarufu Wa Lowassa Waporomoka, Magufuli Apaa

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97.

Lakini utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Researc and Consultant na Ms Midas Touche East Africa kwa kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika kanda sita na mikoa 15, unaonyesha kuwa Magufuli ameongeza umaarufu kwa takriban asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20 pia.

Katika utafiti huo, Lowassa anaonekana kushuka hadi asilimia 20.1.

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Anna Mghwira aliyepata asilimia 1.1, Hashimu Rungwe (0.4), Fahmi Dovutwa (0.2), Lutalosa Yemba (0.1), Janken Kasambala (0.1) na Machmillan Lyimo aliyepata asilimia 0.0. Asilimia 3.5 ya walioulizwa swali hilo walikataa kujibu.

Vilevile, wananchi walipouliza iwapo Uchaguzi Mkuu ukifanyika leo wangemchagua nani kati ya makada waliojitokea kugombea urais mwaka jana, wengi wamemtaja Magufuli.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba wanawake wengi ndiyo wanamuunga mkono Magufuli ikilinganishwa na wanaume.

Asilimia 77.9 ya wanawake wanasema wapo tayari kumchagua tena kuwa Rais iwapo kutakuwa na uchaguzi mpya, wakati wanaume wanaosema hivyo ni asilimia 71.5 pekee.

Kinyume na ilivyo kwa Magufuli, utafiti umebaini kwamba Lowassa anapendwa zaidi na wanaume huku asilimia 22.6 wakisema wapo tayari kumchagua kuwa rais. Ni asilimia 17.4 ndiyo wametoa maoni kama hayo kwa Magufuli.

Kwa upande wa kanda; Kanda ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa ‘kumkubali’ Magufuli ikiwa na asilimia 91.6, ikifuatiwa na Kanda ya Kati yenye asilimia 81.6, Kanda ya Kaskazini (77%), Kanda ya Pwani (72.7) na Kanda ya Ziwa asilimia 67.6.

Alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbuso alisema kuongezeka kwa umaarufu wa Rais Magufuli kunatokana na utendaji wake kugusa kero za wanyonge.

Alisema Watanzania wengi hata wale waliokuwa wakiunga mkono vyama vya upinzani, wameanza kukubaliana na Magufuli kutokana na namna alivyoweza kufanya mambo makubwa na yenye umuhimu kwa Taifa ndani ya muda mfupi.

“Hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa namna hii ndani ya siku 100 ndiyo maana wanyonge wameonekana kumkubali kwa sababu amegusa na kuonyesha wazi nia ya kumaliza changamoto zao,” alisema.

“Hata ikitokea uchaguzi ukafanyika sasa nina uhakika Magufuli atashinda kwa sababu wananchi wamebaini wazi kuwa anachokizungumza ndicho anachomaanisha. Si siasa kama ambavyo imezoeleka kwa wanasiasa wengine.”

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa Tanzania Labour Party na mbunge wa zamani wa Vunjo, Augustine Mrema aliyesema kuwa Watanzania walifanya uchaguzi sahihi kumuweka Magufuli madarakani.

Alisema katika kipindi cha siku 100 kiongozi huyo amefanya miujiza ambayo hakuna Mtanzania ambaye alifikiria kuwa ingeweza kufanyika.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi sana ukweli ni huoooo, asikudangany mtu na ninadhani uchaguz ujao atapat 90% kwan kila mtu atamkubali na hapo upinzan ndo utaporomok kutokan na ujing wanao ufanya ndan ya bunge. Mtu aje akudangany et akishindw atakwend chunga ngo'ombe sasa alisha kwenda? achen bana mwongo ni mwongo tu siku zote na mkweli ni mkweli sikuzote. mtu waina hiyo ukimchagua unafikiria eti atakufanyia yale alio kwambia? laasha, kama anawez kuwafanyizia wanainch bas atimiz ahad yake ya kwend kuchung ngo'ombe ili uchaguz ujao watu wasem kwel huy ni mkweli. Nawaonea hurum upinzan kwan 2020 watasambaratishwa vibaya na JPJM. Honger muheshimiwa. Mimi sio mtanzania na unay yafany sikuamin kwamb unawez yafany kwan nilikua na mkubali MEMBE kumb mtumish ni wewe nakubali unanifany nitamani kua mtanzania.

    ReplyDelete
  2. Asilewe sifa na kubadili mwelekeo wake huyo magu,sisi tunamtizama kwa makini wala hatuangalii sura tunataka kazi

    ReplyDelete
  3. Awamu ya pili tukimchagua asianze kubembea Na yeye maana inakuaga hivyo a kufanya massages ya milioni nne Na laki saba nchi za jirani

    ReplyDelete
  4. Hivi rais WA Tanganyika ni nani uliza wazungu
    Wanasemaje Ni Nyerere

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad