Waliovamia Shamba la Sumaye Watii Amri ya Paul Makonda

Paul Makonda
Wananchi wanaodaiwa kuvamia shamba la Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, lililopo Kinondo, mtaa wa Mji Mpya, kata ya Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni, wametii agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (pichani), la kuwataka kuacha kuendelea na ujenzi katika maeneo waliyogawiana.

Katikati ya wiki iliyopita, mkuu huyi wa wilaya alifanya mkutano na wananchi hao pamoja na Sumaye na kuwataka kutoendelea na ujenzi katika maeneo hayo hadi baada ya wiki mbili atakapokuwa amekutana na viongozi kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kuwasaidia wananchi hao.

Pia Makonda alitaka nyumba zote zilizokwishajengwa katika eneo hilo zihesabiwe halafu apelekewe orodha ya nyumba hizo pamoja na wamiliki wake.

Wananchi hao wakizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa kujadiliana kuhusu agizo la Makonda, walisema hawataendelea na ujenzi wa nyumba zao hadi hapo watakapopata maelekezo mengine kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya kama alivyowataka.

Mmoja wa viongozi wa wananchi hao, Athuman Hassan, alisema wanaheshimu kauli ya mkuu wa wilaya, hivyo hawataendelea na ujenzi wa nyumba zao hadi hapo watakapopata maelekezo mengine.

"Sisi tunaheshimu maelekezo ya mkuu wetu wa wilaya, tumeamua kusimamisha ujenzi wa nyumba hadi hapo tutakapopata maelekezo mengine, hivyo wananchi mnatakiwa kuwa wavumilivu katika kipindi cha wiki tulizoambiwa nina imani na DC wetu atatusaidia kama alivyotuahidi, " alisema Hassan.

Aidha, aliwataka wananchi ambao wameshakamilisha ujenzi wa nyumba zao na kuanza kuishi kuendelea kuishi kwa amani na utulivu katika nyumba zao hizo.

"Wenzetu ambao mmeishakamilisha ujenzi wa nyumba zenu endeleeni kuishi kwa amani na utulivu wakati tukisubiri maelekezo mengine kutoka kwa mkuu wetu wa wilaya kwa ajili ya ambao tulikuwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad